EXCLUSIVE::HISTORIA NZIMA YA MAISHA YA WEMA SEPETU ISOME HAPA
Taja wasichana wote wa Bongo Movies wanaotamba Tanzania, usipoliweka
jina la Wema Sepetu orodha haijakamilika. Wema Sepetu ni supastaa
asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na
websites/blogs. Mfahamu zaidi kwa undani leo anaposherehekea siku yake
ya kuzaliwa katika mahojiano haya aliyoyafanya na Bongo5 kwaajili ya
jarida la Mzuka.Kwenu mko wangapi na wewe ndio mtoto wa mwisho?
Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu. Wa
kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana
familia yake. Wa kwanza yuko kule anafanya kazi ana mtoto mmoja. Wa tatu
yuko kule anasoma na anafanya kazi
Miaka mitano kabla ya mwaka 2006, Wema alikuwa ni msichana wa aina gani?
Wema alikuwa ni msichana wa kawaida. Wakati ule ulikuwa ukiniuliza
unataka kuwa nani ukikua ningekujibu nataka kuwa air hostess sababu
dreams zangu zilikuwa ni kuwa air hostess, sijawahi kufikiria kabisa
kuingia kwenye fame. Though nilikuwa nawaangalia watu kama Ray C,
K-Lynn, Kwasababu mimi nilikuwa nasoma academic na shuleni kwetu
nakumbuka tulikuwa tukitoka ile home time kulikuwa na duka fulani hivi
la mpemba tunaenda tunakula sambusa nini, so magari yatapita nini and we
would see Ray C and everybody will go like ‘you see Ray C’ you know,
kwahiyo we go crazy over superstars na watu famous.
Kiukweli I never so myself kuwa katika this position ambayo niko.
Kwahiyo nilikuwa tu msichana ambaye sina ndoto za kuwa star lakini
nilikuwa tu nawashangaa masupastaa. My dad amekuwa anapenda sana
mashindano ya Miss Tanzania and kila mwaka alikuwa anamake sure kwamba
amenunua tiketi ya kwenda kuangalia Miss Tanzania.
So nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa akina Sylvia Bahame tumekaa nyumbani
amekosa tiketi. Akakaa akasema ‘kumbe ukiwa umekaa nyumbani ndio
unaenjoy vizuri kuliko hata kwenda pale’ akasema ‘one day nawish one of
my beauties hata kama hatoshinda, nikilipia tiketi naenda nikijua kabisa
nimeenda kumlipia binti yangu.
So sikukiweka kichwani hicho kitu lakini after kuingia katika whatever
na nini, so siku nimekaa na dad nikamwambia ‘dad unakumbuka kuna siku
ulisema hivi’ akasema ‘yes I remember’ . Hata Mange Kimambi alivyokuja
kuniapproach, alivyoniona Sleep Way akaniambia kwamba anataka niingie
katika mashindano, nikamwambia kwamba mimi nina wazazi wangu, siwezi
nikaamua tu mimi mwenyewe na mimi nakaa na wazazi, so nilivyoongea na
mama akasema ‘ongea na baba yako’ nikampigia simu baba alikuwa kipindi
hicho Dodoma, akaniambia ‘fanya my beauty nitakusupport’, hakuthink
twice alinipa go ahead kabisa.
Kabla ya Miss Tanzania, ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu Wema
Sepetu, ni vipi Miss Tanzania ilibadilisha maisha yako hasa kutokana na
watu kuanza kufuatilia maisha yako na chochote unachofanya?
Ni kitu ambacho nilikipata bado nina umri mdogo and nilikuwa
sijajiandaa, nilikuwa naichukulia tu poa this whole issue ya kuwa kwenye
spotlight. Nilikuwa sidhani kama itakuwa vile kwasababu kama
wanavyosema experience ni bora uexperience mwenyewe usione kwa wenzako
so nilivyokuwa naichukulia ni tofauti na ilivyokuja kuwa kwasababu mimi
nilikuwa naichukulia tu ‘kuwa star raha’ umeenda watu wamekushangaa nini
lakini nilivyokuwa nimeingia sana katika ile spotlight nikasema kumbe
ooh my God it’s this hard.
Kwahiyo ikawa ni kitu kilichonipa wakati mgumu sana kukizoea like mpaka
sasa hivi naweza kusema kwamba ile umetoka kila mtu kakuangalia nini,
it’s not an easy task, yaani haizoeleki hiyo hali yaani kila siku
unazidi kuiona mpya kwasababu there is no place unaweza ukaenda ukawa na
privacy yako, yaani upende usipende lazima utakuwa ni attention kwa
watu, lazima watu watakuangalia. Sometimes natamani tu na mimi niwe Wema
lakini huwezi sababu all eyes on you. And a lot of times as a normal
human being kuna time unahisi you just be yourself lakini inakuwa ni
time chache chache sana. The only place where I can be myself is in my
room and in my house, out of my gate you cannot be yourself.
Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?
Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba mwenyezi
Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio amenipangia hivi
nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa kila mtu, lakini
siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda mara moja mara
mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi ukapata regrets kama
hakuna tatizo.
Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa Miss
Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa na
pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha hayo
ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?
Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani lakini
hatushei sana zile common interests kama zamani because once upon a time
tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo kwenye
spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao naonana
nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being Miss
Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine
ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare
nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja.
Ulikuwa na boyfriend tayari?
Yes nilikuwa naye
Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?
Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza kusema. Sana
sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend ambaye
unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na
boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no
boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba
nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi
nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia
‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya
kwamba sishiriki.
So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha yangu
kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti kuanzia
naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye gazeti. So
kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ so sikuonana
naye the whole day.
Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa namsikiliza.
Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo
umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’.
Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini
luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu
swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport
mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa
ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye
vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema
tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho
tunaongea, tunasalimiana’
Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?
Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu mimi
nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na mama
yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini
nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa
nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui
nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada
yangu.
Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana protective
kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya pale nyumbani
kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different furnitures, so
tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la Mwanamboka
kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda pale wakati
tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao nini
,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, tumepark
gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya tukasalimiana
akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na mimi napenda
unavyoigiza’ nini na nini.
Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’.
Nikamwambia siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle Hashimu
wataniua wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila
kuwaconsult so akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati
ananiambia tuachie nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja
umemuona Wema?’ Aliniringia sana.
‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia poa,’Kaka basi
chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza tukamtumia
kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani. Basi
nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza, ‘Hee
Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao.
Basi, so baada ya hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep
nikamsave, basi mimi nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba
inanipigia ambayo nimeisave vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’
akaniambia ‘vipi, safi Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’
‘haya basi sawa basi baadae’ nikamwambia ‘poa’.
Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext ‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi uko
wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia ya kutextiana kila siku
tunandelea for one weak tunatext mara yeye ataniuliza umekula nini, mara
sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu unajua kwamba mwanaume akiwa
ana interest na wewe. Kidogo tukaanza kuulizana una boyfriend una
girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia mimi ‘nipo kambini Lamada’
akanielekeza nikafika.
Basi nimefika siku hiyo tumekaa pale garden akaniambia ananipenda na
nini, hivyo. Kipindi hicho nilikuwa sina boyfriend nilikuwa very very
single, so nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na boyfriend wangu sijui
nini’ akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie basi’ Nakumbuka
tulivyokuwa tunaondoka ndo tukakiss, it was our first kiss. Basi
nikaondoka, akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia siwezi
akaniambia please, please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia ‘sawa’
basi nikarudi then akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi
yakaanza.
Basi kwenye mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact movies na
wewe’ nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi unaweza
kuact hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia
‘unaweza kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’
akaniambia ‘basi kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu
ukimenya si unalia, basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ .
Akaniambia niende kuonana na bosi wake. Nilivyofika tu ofisini nikaonana
na Mtitu Game. Akanipa script akaniambia nikasome kama story akaniambia
‘wakati unasoma uwe unasoma sana concentrate kwenye Dina. Basi vile
tukiwa tukikutana tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa basi wewe you
are ready to shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, hauwezi amini, I
just felt yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa wengine wanaona it’s
hard unajua.
Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back to
school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka ya
International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu ya
Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona kwamba
kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo soon
naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’
Nimerudi kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White Maria
yaani tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa
nimeshajikuta katika movie, so that why I keep saying kwamba without him
nisingejua.
Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika mahusiano yako
yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?
Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi
kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana,
so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo,
nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na
rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua
vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa
naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa
ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu).
Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio
ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda
Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala
ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just
from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na
hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya
vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio
sana tunajuana tu.
Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party
tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda.
So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna
mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa
amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.
Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja
nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz
nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No
mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo
Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha
nimalize issue ya London halafu nitakuambia.
Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia
Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa
ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz.
Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi wakati
nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui
yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha
nikumuuliza anakataa.
Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya
siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema,
basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa
mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana
na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu
nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia
simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja
yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona
tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana,
nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia
I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi
no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb
tukaanza kuishi pamoja.
Mwaka jana alipooenda kutumbuiza kwenye Big Brother Africa, alidai kuwa
ameweza kuongea Kiingereza kwasababu yako, ulikuwa ukimfundisha ama
ulikuwa ukipenda kumuongelesha Kiingereza zaidi?
Yes. Naseeb alikuwa hajui Kiingereza, alikuwa anajua cha juu juu. Ila
mimi na Naseeb tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume. So mimi
nilivyo kidogo nimetupia Kiingereza kwahiyo hiyo ilikuwa inampa tabu
kwenye the first two months kwahiyo most of the times nikawa naongea
naye Kiingereza. Lakini he is smart, Naseeb is very smart yaani akiwa
haelewi kitu ‘hivi baby hapa kwenye has na have unafanya nini, hapa
natumia tense gani? Niweke ing niweke nini?’ mwisho wa siku nikajikuta
like tunatumia most of the time kufundishana. Akisema kitu ambacho sicho
namwambia ‘usije ukarudia tena kusema hivyo mbele za watu watakucheka’.
So akajikuta tu anaweza.
Kwanini mliachana?
Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate .Nilikuwa
sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza
kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him
na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na
maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini
tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari
nimesharidhika naye.
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or
another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka
kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini
kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi
Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka,
nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari
yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale
nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka
zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana
napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala
mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki
kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada
yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha CREDIT : BONGO5
0 comments:
Post a Comment