HIZI NDIZO SABABU 3 NDOA YA VICKY KAMATA KUYEYUKA
Vicky Kamata akiwa katika pozi na mwanaume aliyepanga kuoana naye anayejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.
KATEKISTA AZUNGUMZA NA IJUMAA WIKIENDA
Hadi
gazeti hili linaondoka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria
Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10:00 jioni, ndoa ya Mbunge
Vicky Kamata iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka.
Vicky
Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa
Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles
wa jijini Dar.Baada ya kuona muda unakwenda bila kuwepo kwa
dalili za wahusika kufika kufunga ndoa hiyo ambayo harusi yake ilidaiwa
ingetumia shilingi milioni 96, wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko,
Cuthbert Maganga ili kumsikia anasema nini kuhusu hilo.
Hata hivyo, mtu aliyedai ni katekista wa kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija, Buguruni, Dar.
Kuhusu
ndoa ya Vicky Kamata, katekista huyo alidai Jumapili ya Mei 18, 2014
ndani ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani ‘laivu’ kwamba
haitafungwa.
Vicky Kamata akiwa amelazwa baada ya kuugua ghafla katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar.
SABABU ZA KANISA
Habari za ndani zilidai kuwa kanisa lilibaini upungufu mkubwa kwa bibi harusi na kumwambia ndoa haitakuwepo.
Upungufu
huo ni pamoja na Vicky Kamata kushindwa kuwasilisha cheti chake cha
ubatizo, pia hakuwahi kupata kipaimara. Ilidaiwa kuwa vitu hivyo kwa
uchache wake ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la Sakramenti ya
Ndoa.
SABABU ZA NDANI
Ukiachana
na sababu hizo za kanisa, Ijumaa Wikienda lilichimbua na kubaini sababu
kuu 3 ambazo zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa ndoa hiyo.
Vicky na Charles wakila bata.
SABABU YA KWANZA
Kwa
mujibu wa chanzo, mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa
nyingine ya kanisa na imejaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa
rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume
mmoja mke mmoja mpaka kifo kiwatenganishe.
MKE ATINGA BUNGENI
Chanzo
kilizidi kudai kuwa wiki iliyopita, mwanamke huyo ambaye jina
halikupatikana, alitinga bungeni na kuonana na Spika wa Bunge, Anne
Makinda ambapo alijitambulisha ndiye mke wa Charles anayetaka kufunga
ndoa na Vicky Kamata.
“Mke wa bwana harusi alikuja Dodoma juzi, akasaidiwa kuonana na spika na mbunge mmoja (jina tunalo).
“Alimwambia
spika yeye ndiye mke wa ndoa wa Charles, ila walitengana. Lakini
alisema pamoja na kutengana huko, ndoa ya Kikristo haifungwi mara mbili
labda mmoja afe. Kwa hiyo mumewe hawezi kufunga ndoa na Vicky,” kilisema
chanzo.
SABABU YA PILI
Sababu
ya pili ilielezwa kuwa, Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani
mwanaume huyo alishatoa mahari kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa
jijini Dar na ukweni anajulikana.
“Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana.
“Sasa
ilipotoka ile picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa
(Mei 16, 2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky itatumia shilingi
milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule msichana na ukweni, ndiyo jamaa
akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA TATU
Sababu
ya tatu ilitajwa ni kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky
aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar
kwa hiyo isingekuwa rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake
kuwa mbaya.
WAANDISHI WATINGA HISPITALI
Ijumaa
iliyopita, waandishi wetu walitinga kwenye hospitali hiyo na kukutana
na daktari mmoja ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo lakini alikataa
waandishi wasimuone kwa sababu hayuko katika hali nzuri kiafya. “Ni
kweli Vicky kalazwa hapa lakini hamuwezi kumwona, hayuko katika hali
nzuri, anahitaji kupumzika jamani, please,” alisema daktari huyo.
HATIHATI ILISHAKUWEPO
Katika
Gazeti la Uwazi la Mei 20, 2014 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari
ndogo yenye kichwa kisemacho; NDOA YA MIL. 96 YA VICKY KAMATA HATIHATI
KUFUNGWA.
Katika habari hiyo ilielezwa kuwa ndoa hiyo isingefungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe kibao.
Habari
za ndani zilisema mizengwe hiyo iliibuka katika hatua za mwisho na
kusababisha mwanaume kuamua kubatilisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe
Mei 24, mwaka huu jijini Dar.
KIONGOZI MKUBWA SERIKALINI
Ilidaiwa
kuwa baada ya kuibuka kwa zengwe na mume kutangaza ndoa basi, Vicky
aliumia na kuzifikisha habari hizo kwa Spika Makinda ambapo naye
alizifikisha kwa kiongozi mmoja mkubwa serikalini, hasa bungeni.
Kiongozi
huyo alichukua jukumu la kumvutia waya bwana harusi na kumsihi
kutochukua mawazo hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini mwanaume huyo
alikataa katakata akisema mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo
yaachwe kwenye familia.
MAMA SITTA ASIKITIKA
Habari
zinazidi kusema kuwa kati ya watu ambao wamehuzunishwa na kutofungwa
kwa ndoa hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), mheshimiwa Margaret
Simwanza Sitta ambaye aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo alisikitika si
kwa sababu alikuwa kwenye vikao vya harusi, bali pia aliuona wakati
mgumu atakaoupata Mhe. Vicky.
WABUNGE WAULIZIA MICHANGO YAO
Pamoja
na yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge
waliochanga pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza
kuulizia michango yao wataipataje kwa vile harusi basi tena!
“Huku
Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia
michango yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema
mbunge mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.
WABUNGE WATAJWA KUINJINIA
Mbunge
huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kuna wabunge wametajwa
‘kuinjia’ zengwe la kutokufungwa kwa ndoa hiyo kwa sababu wanazozijua
wao ambazo Ijumaa Wikienda haikupewa lakini inaendelea kuzichimba.
VICKY KAMATA
Vicky alipotafuwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote kuhusu kuyeyuka kwa ndoa yake hakupatikana hewani.
0 comments:
Post a Comment