HOSPITALI YA MT MERU YAKABILIWA NA UHABA WA MASHUKA
siku.
Akizungumzia upungufu huo juzi hospitalini hapo, wakati akipokea msaada wa shuka nyeupe 100 na blanketi 30 toka kwa Kanisa la Calvary
Temple la Kilombero Jijini Arusha,ambalo linaadhimisha miaka 75 tangu lianzishwe, Mganga Mfawidi wa Hospitali hiyo, Dk. Josiah Mlay, alisema
upungufu ni mkubwa wa vitu hivyo ukizingatia wanakwenda kipindi cha baridi kali.
Alisema
kuwa shuka na blanketi walizonazo kwa sasa nyingi zimechakaa kutokana
na kemikali wanazotumia kufulia wakati zinapochafuka wodini,
hivyo wanahitaji shuka na blanketi zingine haraka kabla ya msimu wa baridi haujaanza.
hivyo wanahitaji shuka na blanketi zingine haraka kabla ya msimu wa baridi haujaanza.
“Kwa
nyie kutuletea hivi vitu tunashukuru sana na mtabarikiwa, kwani bado
tuna upungufu wa itu hivi mkubwa na tunaomba wadau wengine
wajitokeze kutusaidia kabla ya msimu wa baridi haujaanza,”alisema.
wajitokeze kutusaidia kabla ya msimu wa baridi haujaanza,”alisema.
Dk.
Mlay alisema kwa sasa hospitali hiyo inachangamoto kubwa ya ongezeko la
wagonjwa na huku mahitaji yao yakipungua, kutokana na
wingi wao, hivyo wanahitaji wasamaria wema wajitokeze kuwasaidia. Mahitaji mengine wanayohitaji hospitalini hapo alitaja kuwa pamoja na
vifaa vya maabara navyo ni vichache,hivyo wanaomba msaada kwa wasamaria wema na sio kuiachia serikali ambayo inamajukumu mengi. Kwa upande wake Emmanuel Mbwiga ambaye ni Mzee wa Kanisa la Calvary

Temple
la Kilombero Jijini Arusha, akitoa msaada huo alisema mbali na msaada
huo pia kupitia vituo vyao mbalimbali wametoa msaada kwenye
vituo vya yatima vya Huruma Kwamurombo,Monduli,Esso.
vituo vya yatima vya Huruma Kwamurombo,Monduli,Esso.
Pia
misaada mingine imetolewa shule za msingi Mwangaza, Olsinyai Sombetini
na Ngarenaro, lengo kubwa kusaidia watu wenye shida ili
wapate faraja nao katika kuadhimisha kilele cha kanisa hilo kitakachofanyika Kitaifa Mbeya Julai mwaka huu.
wapate faraja nao katika kuadhimisha kilele cha kanisa hilo kitakachofanyika Kitaifa Mbeya Julai mwaka huu.
Mbwiga
alisema vitu walivyotoa maeneo hayo ni Sabuni, ndoo za mafuta, mchele,
nguo, mahindi,daftari,soksi na vitu vingine vingi, ambavyo
vyote vina jumla ya shilingi milioni 3.
vyote vina jumla ya shilingi milioni 3.
Hata
hivyo alitoa wito kwa watu wenye mapenzi mema kujitokeza kusaidia
hospitali hiyo na maeneo yenye uhitaji kama vitruo vya yatima
na shuleni, ili wabarikiwe zaidi.
na shuleni, ili wabarikiwe zaidi.
0 comments:
Post a Comment