INASIKITISHA::MTOTO SHIGELA ALIYEZALIWA NA VVU AAGA DUNIA JIJINI MWANZA
Mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akifurahi na Marehemu Shigela enzi za uhai wake.
Marehemu Shigela ezni za uhai wake akihojiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.
Mtoto Shigela amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 29/05/2014 nyumbani kwao mkoani Mwanza akisumbuliwa na maradhi ya Moyo.
Mtoto Shigela alikuwa ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na VVU na kipindi cha Mimi na Tanzania kilimtangaza na alipatiwa misaada mingi toka kwa Watanzania .
Bado msaada wako unahitajika kukamilisha mipango ya mazishi kwa mtoto wetu mpendwa Shigela.
Namba ya simu ya dadake Shigela 0758343178.
Bwana ametoa na bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe.
0 comments:
Post a Comment