Friday, 30 May 2014

:Arsene Wenger: Wachezaji mashoga wa Premier League wasijitangaze


 Meneja wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa wachezaji mashoga wa Premier League hawatakiwi kujitangaza wakati wa maisha yao ya soka
kwa sababu ya kuhofia kushushwa thamani. Kiungo wa zamani wa Aston Villa Thomas Hitzlsperger alijitangaza mapema mwaka huubaada ya kustaafu kucheza soka. "Kwa sababu ya matakwa ya vyombo vya habari, labda hakuna atakayejitangaza," amesema Wenger. "Hakuweza kujitangaza wakati anacheza ikimaanisha tuna maendeleo zaidi ya kufanya soka lisogee." Matamshi ya Wenger yanakuja kufuatia yale yaliyotolewa na mchezaji wa zamani wa Leeds Robbie Rodgers,ambaye amesema ilikuwa "haiwezekani" kujitangaza halafu ukabaki kwenye soka. Kama ilivyokuwa kwa Hitzlsperger, Rodgers alijitangaza baada ya kumaliza masuala yake ya soka.
Lakini hata hivyo mchezaji Liam Davis amejitangaza na akaendelea kucheza soka. Na kwa upande wa soka la wanawake, Casey Stoney ameendelea kucheza kwa kiwango cha juu katika klabu yake ya wanawake ya Arsenal Ladies na England baada ya kuweka wazi masuala yake ya ujinsia mapema mwaka huu. Wenger, akizungumza na Arsenal Magazine kuhusu masuala ya mahusiano ya jinsia moja katika soka,amesema siku ambayo ambayo masuala ya mapenzi ya jinsi moja ya mchazaji hayakuwa tatizo, mpira wa miguu uliuwa na njia. "Hitzlsperger asingweza kusubiri mpaka mwisho wake," ameongeza. "Lakini yote hakutakiwa kujitangaza kwa sababu angalitafsiriwa kama jambo lingine. "Inaweza kuwa vizuri kwa watu wanne, watani, sita kujitangaza na baada ya hapo hakuna hata mtu mmoja atakayezungumzia kuhusu kwa sababu wanafikiri kwamba ni watu ambao wanaishi maisha yao kama ambavyo wanatakiwa kuishi. "Nadhani mpira wa miguu upo kwa ajili ya kukasirisha vipimdi vya furaha, kuburudisha na kuleta athari chanya kwa watu, haijalishi wapi wanakotoka, rangi yao ya ngozi iko namna ganie, wana dini gani au wanapenda mapenzi ya namna gani. "Inahuzunisha sana kwamba baadhi ya watu hudhani kwamba mchezo huu unatakiwa kuchezwa na watu fulani ambao wana tabia fulani. Iko wazi kwa kila mtu anayependa mpira wa miguu na hiyo isipotokea, haikubaliki." Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika kundi linaloongoza kudai haki za mashoga barani Ulaya, Stonewall, ambalo lina jumla ya mashabiki 30,000 kutoka nchi 29, imebainika kwamba mashabiki wa soka wa Ireland watawakubali wachezaji wa timu yao ya taifa kama watajitangaza kuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ambapo 83% wanasema wako sawa na wazo hilo. Sweden na Denmark zinafuatia kwa 79% mbele ya United Kingdom yenye 73%, wakati waandaaji wa Kombe la Dunia mwaka huu, Brazil wako nafai ya sita kwa 67%. Mashabiki kutoka nchi za Kuwait na United Arab Emirates zote zina 7% ikiwa ni kiwango cha chini kabisa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA