MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU FROSSIE CHIYAONGA ALIYEKUWA BALOZI WA MALAWI NCHINI.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini
Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa
kuelekea Malawi kwa maziko
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu,
Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania,
aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji baadhi ya wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa
Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za
kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Malawi wakati wa
shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania.
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.
Sehemu ya waombolezaji mabalozi wa nchi mbalimbali waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa
heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie
Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki
ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa
marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es
Salaam, leo Mei 12, 2014.
Picha na OMR
0 comments:
Post a Comment