JACQUELINE WOLPER ALEWA HADI KUANGUKA UKUMBINI...NI NOMAA...CHEKI HAPA
Staa wa
sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuwa tilalila na
kujikuta akipiga mwereka kwenye shughuli ya kibao kata cha mwigizaji
mwenzake, Vanita Omary.
Kwa mujibu
wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio hilo lilijiri
kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani FM Club), Kinondoni jijini Dar ambapo
mastaa kibao walihudhuria.
Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.
Mbali na
pombe pia alikuwa kivutio kwa staili ya ukataji wake wa mauno akiwa na
kivazi kilichoacha nje mapaja yake akiwa na rafiki yake aliyetajwa kwa
jina moja la Vivi.
Katika hatua
nyingine, Vanita alijikuta akiangua kilio baada ya wapiga ngoma wa
kibao kata ‘kuwa feki’ na kushindwa kufanya kazi kama walivyoahidi.
Kutokana na
hilo, baadhi ya mastaa kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’
waligoma kucheza na kukizomea kibao kata hicho ambacho kililetwa na MC
(jina linahifadhiwa) akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na wana ufundi wa
hali ya juu.
na BS
0 comments:
Post a Comment