Tuesday, 27 May 2014

Mtumishi wa idara ya Afya Afia Gesti


Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo
Mwili wa Marehemu Munuo ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama
Mtumishi wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa kahama, Mkoani Shinyanga, Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya kulala wageni mjini Kahama. 

Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama. 

Taarifa zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu. 

Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi. 

Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
 
NA farajimfinanga.com

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA