Wanajeshi wa Kenya wauwa na Al Shabaab
Serikali
ya Kenya imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wa jeshi wameuawa na
wengine wawili kujeruhiwa, baada ya wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shaabab
kufanya shambulio la kuvizia, baada magari yao kukwama barabarani huko
Somalia.
Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.
Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea.
Kamanda wa polisi mjini Mombasa Robert Kitur amethibitishia BBC kuwa shambulio hilo limetokea.
Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus'ab amedai kuwa wapiganaji wake walifanikiwa kuteketeza magari kadhaa ya jeshi la Kenya, madai ambayo yamekanushwa vikali na utawala nchini kenya.
Aidha amesema wa wapiganaji kadhaa wa Al shabaab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.
CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment