MAUAJI YA KUSIKITISHA WAMACHINGA WAMUUA ASKARI
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana wanaodaiwa ni Wamachinga wamemuua askari mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga na stuli kichwani wakati akitimiza majukumu yake.Marehemu Stephano Benjamin Komba (36) ambaye aliyekuwa na cheo cha sajenti.
Akizungumza
na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Taifa
Muhimbili wakati wa kuuaga mwili huo, Mkuu wa Oparesheni Manispaa ya
Ilala, Charles Wambura alimtaja marehemu kwa jina la Stephano Benjamin
Komba (36) aliyekuwa na cheo cha sajenti.
Alisema tukio hilo lilijiri Mei 16, mwaka huu, saa 7.30 mchana kwenye Mtaa wa Raha Kariakoo.
“Marehemu
alikuwa na askari wengine walikamata baadhi ya bidhaa za Wamachinga kwa
lengo la kuwaondoa lakini ghafla walivamiwa na kundi la wafanyabiashara
hao ambapo Sajenti Komba akapigwa kichwani kwa stuli hali iliyomfanya
apoteze fahamu kwa kuvuja damu nyingi.
“Askari walipambana na hao Wamachinga na kufanikiwa kumuokoa Sajenti Komba lakini akiwa na hali mbaya.
Mke wa Marehemu Stephano Benjamin (katikati) akisaidiwa na jamaa wa karibu msibani kumuaga marehemu mume wake.
“Walimkimbiza
Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya
ndipo walimpeleka Muhimbili ambapo alifariki dunia saa 2:00 usiku,”
alisema Wambura.
Mwili wa marehemu uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mbagala na kusafirishwa kwao Songea, mkoani Ruvuma kwa mazishi.
Wambura
aliongeza kuwa, hakufurahishwa na kitendo hicho cha Wamachinga kuchukua
sheria mkononi.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi
alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutii sheria bila
shuruti.
na GPL
0 comments:
Post a Comment