ANGALIA PICHA KIJANA ASHUSHIWA KIPIGO CHA MBWA AKIDAIWA MWIZI KABLA YA KUGUNDULIKA KUWA HANA HATIA
Kijana mmoja aleyetambulika kwa jina moja la sule amenusurika kifo baada ya kupingwa na watu wenye asira kali wakimtuhumu kuwa ni mwizi jambo ambalo baadae lilikuja kubainika kuwa hana hatia yoyote.
Wakizungumza eneo la feri jijini dar es salaam baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa inasikitisha kuona watu wakijichukulia sheria mikononi bila kuhoji tukio ambapo mara baada ya kipigo ambacho kimemsababishia majeraha makubwa kijana huyo hakuna mtu aliye jitokeza kulalamika kuibiwa wala kujulikana kijana huyo ameiba nini.
Akiongea kwa shida kijana huyo amesema kuwa yeye hakuiba chocho na hajui kwa nini watu walimvamia na kuanza kumpiga
Katika hatua nyingine ya kujaribu kunusuru maisha ya kijana huyo baadhi ya wasamalia wema waliamua kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya usalama lakini mara baada ya kumfikisha katika kituo kidogo kilichopo karibu na hapo walikuta kituo hicho kimefungwa na kufuri na hakuna askali yoyote lakina baada ya muda askali polisi mmoja alitokea.
0 comments:
Post a Comment