Monday, 2 June 2014

BIBI WA 'MTOTO ALIYEISHI KWENYE BOKSI' ALIMLILIA MJUKUU WAKE


Bibi wa mtoto Nasrah Rashid, Bi. Asha Abdallah akilia kwa uchungu baada ya kupata taarifa za msiba wa mjukuu wake huko nyumbani kwake maeneo ya Mafisa mkoani Morogoro. Kushoto ni mwanae Khadija Hamisi.

Bi. Asha akiwa na simanzi kwa kuondokewa na mjukuu wake Nasrah aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi. 

Baba wa mtoto Nasrah, Rashid Mvungi (47) akiingizwa mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto Nasra.
Nasrah Rashid enzi za uhai wake.
Watuhumiwa wengine kwenye sakata hilo mama mlezi, Mariam Said (38) wa kwanza kushoto na mume wake Mtonga Omar (30) wa kwanza kulia wakisindikizwa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi baada ya kusomewa mashitaka.
MTOTO Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia.



 Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki. 


Tunalaani vitendo hivi vya kikatili alichofanyiwa mtoto huyo licha ya madaktari kujitahidi kuokoa maisha yake lakini mungu ameamua kumchukua....

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA