Monday 30 June 2014

DAVIDO TENA:ATWA TUZO YA BET ILIYO KUWA IKIWANIWA NA DIAMOND! SOMA WALICHO KIANDIKA!


Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani....Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo... Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa... Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi!.... Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa.....!!!!!! @wcb_wasafi For Life Baby ������
 
KUHUSU DAVIDO NAYE........
Screen Shot 2014-06-29 at 9.07.09 PMHii ilikua siku nyingine muhimu kwa Tanzania na Africa kwa ujumla ambapo yalikua yanasubiriwa matokeo ya tuzo ya BET sanasana kipengele wanachowania tuzo wasanii wa Afrika akiwemo Diamond Platnumz.
Davido kutoka Nigeria ndio amethibitisha kuwa mshindi wa tuzo hii ambapo kupitia page yake ya Instagram amewashukuru mashabiki na kuelezea furaha yake.
Tuzo hii ilikua inawaniwa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Mafikizolo wa South Africa, Sarkodie wa Ghana, Tiwa Savage wa Nigeria na Toofan wa Togo.
Pamoja na kwamba Diamond hajawa mshindi wa tuzo hii, Watanzania wengi wamekua upande wake toka alipochaguliwa kuwania tuzo hizi na kumwambia hata kama hatoshinda, kuchaguliwa tu kushiriki BET ni zawadi ya kipekee na hatua kubwa kimuziki.
Namkariri Rais Jakaya Kikwete pia aliesema ‘Hata kama asiposhinda Diamond, yenyewe kuchaguliwa kwenye tuzo za BET ni hatua kubwa kimuziki’
Screen Shot 2014-06-29 at 9.13.38 PM

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA