MWILI WAKO USITUMIKE KAMA SHUKRANI KWA WANAOKUSAIDIA
Najua 2024 imekuwa mchaka mchaka sana lakini kuona hadi sasa unaishi ni wazi kuwa Mungu bado ana mpango na wewe sasa kwa moyo ya shukrani tukimuomba YEYE tujipange na 2025 ili usiwe mwaka wa lawama bali mafanikio tele...
Sasa turejee kwenye moja na mbili ya leo maana hii homa iliyonikung'uta imenifanya muhubiri....
Sote tunajua katika penzi la kweli kuna kujaliana katika shida na
raha na kuonyesha upendo wa mtu kwa mwenzake.
Tunajua wote katika mapenzi kuna kupendana ili kukamilisha pea ya
upendo ikimaanisha kila mmoja ampende mwenzake kwa dhati.
Penzi la upande mmoja tumeona si kamili kwa vile mpendaji huwa
mmoja na mwingine huwa yupo na mwenzake kwa sababu fulani, akishakidhi haja zake huondoka bila
kwa heri na kusababisha mateso kwa mmoja.
Kuna tatizo limejitokeza kwa kina dada kuamini mtu anayempa msaada
basi anamhitaji kimapenzi. Kweli anayekusaidia lazima atakuwa mtu anayejua utu
wa mtu bila kuangalia anakujua au la (japo wanaotoa msaada wakiwa na lao jambo wapo).....
Sehemu hii imekuwa ikiwachanganya wengi na kuingia kichwakichwa
mwisho kuachwa njia panda na kuona umegeukwa, yaani mtu uliyemuamini
amekugeuka.
Kwa nini?
Upendo na msaada ni vitu viwili tofauti, msaada umo ndani ya
upendo kwa maana anayekupenda atakusaidia katika shida na raha, lakini si kila
msaada una upendo.
Kwa sababu gani?
Mfano; Tumeona kwenye usafiri wanawake wamekuwa dhaifu pale
wanapopewa msaada na mwanaume na huamini msaada ule ni dalili za kupendwa, kumbe aliyetoa msaada hakutoa kama
sehemu ya kuonyesha anakuhitaji kimapenzi bali kukusaidia kama mwanadamu
mwenzake.
Wanawake wengi wamekuwa wakipoteza dira ya maisha kwa kuanzisha
uhusiano na mtu anayekutana
naye safarini na kumpa msaada kama chakula au kumsaidia mtoto.
Baada ya msaada huo mioyo yao huwa dhaifu na kuamini yule ndiye
mwanaume sahihi kwa vile kamsaidia bila kumjua pengine msaada huo haupati kwa
mwenza wake.
Mara moja huanzisha uhusiano na kupeana namba za simu ili
watafutane baadaye. Wanawake
wengi hufikia hatua ya kuzikana ndoa zao kwa vile tayari mioyo yao
imeishakurupuka bila kufikiri.
Wengi wao wamekuwa wakifunga hata safari kuwafuata watu hao hata
kama ni mbali bila kuijua historia ya mtu waliyekutana naye kwenye gari.
Baada ya kukutana ndipo wanapokutana na tabia tofauti na
waliyoifikiria, hapo ndipo yanakuja majuto. Wapo wanaodiriki kuvunja hata
uhusiano wao kwa penzi la mwanaume wa safarini na kuamini aliyekuwa naye si
lolote si chochote kwa mwanaume aliyekutana naye.
Hata kama hakumfuata, hicho huwa chanzo cha nyumba kuvunjika au
kuingia kwenye migogoro kwa vile akili yao wameihamishia kwa mwanaume
wasiyemjua.
Baada ya kuachwa anaangukia pua kwa vile yule mtu aliyetoa msaada
haukuwa kwa lengo ya kumvuta kimapenzi.
Hivyo, inatakiwa tuwe makini sana na uamuzi wetu wa kukurupuka, si kila msaada unaopewa asante yake
ni kumvulia nguo mwanaume.
Utawavulia nguo wangapi watakaokusaidia? Kumbuka kusaidiwa ni haki yako kama mwanadamu na si kwa
ajili ya kudhalilishwa.
Kwa Upande mwingine wanaume nao wameshindwa kuelewa kuwa siyo kila msaada na tabasamu kutoka kwa mwanamke nyuma yake kuna sauti ya NAKUHITAJI. Sikatai matendo huongea zaidi ya maneno lakini tusikurupuke kuchosha hisia zetu bila ya kujipa muda kutafakari.
Uheshimu utu na mwili wako, kwa sababu heshima ya mtu huijenga
mwenyewe hujengewi na mtu. Usikubali
kuutoa mwili wako kama asante kwa msaada utakaopewa, asante ya mdomo inatosha.
Kama mtatongozana hiyo ni hiyari yenu kukubali au kukataa, uwe muwazi ili kujiweka eneo salama kwa
kuheshimiwa na si kuukana uhusiano wao kwa vile tu umenunuliwa chipsi na kuku
pengine soda na kitafunwa.
Akitoa ni kwa upendo wake una haki ya kukubali au kukataa si kila
upewacho lazima ukubali kuchukua na asante yako ni kuutoa asusa mwili wako!
0 comments:
Post a Comment