Friday 11 July 2014

BREAKING::MASHAMBULIZI MENGINE YATOKEA LAMU



Mashambulizi yalitokea mara ya kwanza katika eneo la Mpeketoni ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa
Watu waliojihami wamevamia kijiji cha Pandanguo katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya.
Chifu wa eneo hilo Karisa Charo Karisa, anasema kuwa shule na nyumba nne ziliteketezwa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa usiku wa kuamkia leo.
Kwa sasa hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi wa mashambulizi hayo.Duru zinaarifu kuwa washambuliaji hao waliiba bunduki kutoka kwa watu polisi wa dharura na kufanya mashambulizi hayo.
Duru zinasema kuwa washambuliaji hao waliiba bunduki sita kutoka kwa polisi wa dharura kabla ya kuteketeza nyumba.
Kwa sasa hakuna taarifa zozote kuhusu majeruhi.
Inaarifiwa kuwa wanajeshi wamepelekwa katika eneo hilo kudhibiti usalama.
Mnamo mwezi Juni watu watano waliuawa katika eneo hilo la Pandanguo ambalo liko umbali wa kilomita 30 kutoka Mpeketoni ambako mashambulizi mengine yaliwaacha watu zaidi ya sitini wakiwa wameuawa.
Waathiriwa wengi wa mauaji walipatwa wakiwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo na koo zao zikiwa zimekatwa.
Eneo la Lamu ambao liko Pwani ya Kenya limekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara tangu mwezi Juni huku watu wakiuawa kwa misingi ambayo bado ni tata.
Mashambulizi ya Kwanza yaliyofanyika mjini Mpeketoni, yalisemekana kufanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab ingawa serikali alilalaumu wanasiasa kuyachochea mashambulizi hayo.
NA BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA