Sunday 13 July 2014

DAYNA NYANGE AFUNGUKA ,AELEZEA CHANGAMOTO ANAZOPATA BAADA YA KUJICHUBUA


Mwimbaji wa kike Dayna Nyange azungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi baada ya kuamua kubadili rangi ngozi yake na kuwa nyeupe.
Dayna ameeleza kuwa amekuwa akisolewa na watu wengi huku wengine wakitumia lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni watu wanaompenda.

  Ni sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila binadamu anajua jinsi ya kupresent kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.
Amesema Dayna Nyange.
Ameeleza kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili kama tatizo kubwa.
Mwimbaji huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama alivyoamua yeye.
  Kwa hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka Lol..’nimeacha.!
Siwezi kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.
Ameaongeza.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA