MAAJABU::MTOTO AZALIWA NA MIGUU MITATU, ATARAJIWA KUFANYIWA UPASUAJI
Mtoto mdogo ambaye amezaliwa na miguu mitatu amesafirishwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kuondoa miguu miwili
Ana Paula mwenye miezi 22 alikuwa ni pacha aliyeungana ambapo dada yake hakuweza kupona wakati wa upasuaji wa kuwatenganisha.
Ni mguu mmoja tu wa mtoto huyo unaofanya kazi hivyo upasuaji atakaofanyiwa katika moja ya hospitali za watoto ni kuondoa miguu miwili ambayo haifanyi kazi na kumwongezea uwezo wa viungo vyake kufanya kazi.
Ana na mama yake walisafirishwa kutoka Panama kwa msaada waliopatiwa na wasamaria ili zoezi zima liweze kukamilika.
0 comments:
Post a Comment