ANTI LULU: NATAKA KUZAA NA DIAMOND
09:12 |
No Comments |
Msichana wa mjini asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.
BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.
MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).
“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti Lulu.
Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.
Anti Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali japokuwa hawajawahi kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba walishakutana na kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii...
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Niliambiwa alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni zuri hivyo naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye aliwahi kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.
BIFU?
Anti Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba Wema atakasirika, hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha naye bifu zito.
Alisema kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba kikubwa anataka kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja aendelee na maisha yake.
NENO!
“Najua Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa sababu nimeamua na yeye ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito aliyekuwa mpenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda mfupi ilidaiwa kuchoropoka.Pia aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema ambaye naye ilidaiwa ilichoropoka.
Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
SWALI LENYE HOJA!
Baadhi ya watu waliomsikia Anti Lulu akitangaza ishu hiyo walijiuliza swali moja tu: ‘Hivi kweli Anti Lulu huyuhuyu anaweza kuwa mama bora?’Diamond hakupatikana ili kufikishiwa ujumbe huo na kujua namna alivyopokea taarifa hiyo ya Anti Lulu.
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada azae naye.
MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).
“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” alisema Anti Lulu.
Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na Diamond.
Mkali wa Bongo Fleva 'Diamond Platinum' akiwa na mpenzi wake wema Sepetu.
IMANIAnti Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali japokuwa hawajawahi kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba walishakutana na kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii...
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Niliambiwa alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni zuri hivyo naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye aliwahi kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.
BIFU?
Anti Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba Wema atakasirika, hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha naye bifu zito.
Alisema kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba kikubwa anataka kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja aendelee na maisha yake.
NENO!
“Najua Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa sababu nimeamua na yeye ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito aliyekuwa mpenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda mfupi ilidaiwa kuchoropoka.Pia aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema ambaye naye ilidaiwa ilichoropoka.
Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
SWALI LENYE HOJA!
Baadhi ya watu waliomsikia Anti Lulu akitangaza ishu hiyo walijiuliza swali moja tu: ‘Hivi kweli Anti Lulu huyuhuyu anaweza kuwa mama bora?’Diamond hakupatikana ili kufikishiwa ujumbe huo na kujua namna alivyopokea taarifa hiyo ya Anti Lulu.
Read more: http://www.vitukovyamtaani.com/2014/09/anti-lulu-nataka-kuzaa-na-diamond.html#ixzz3Cha8SPju
Related Posts:
MWANAMUZIKI AMIGOLAS AZIKWA LEO MAKABURI YA KISUTU, DAR!CHEKI PICHA HAPA Mwili wa marehemu, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ ukiwasili nyumbani kwao Mburahati leo jijini Dar es Salam. Mjane wa marehemu, Bi Modesta Emmanuel akiw… Read More
AFYA YA VENGU MSANII WA ORIGINAL COMEDY ALIYEUGUA TANGU 2011 YAANZA KUIMALIKA, SOMA HAPA. Msanii staa wa Kundi la Orijino Komedi ‘OK’, Joseph Shamba ’Vengu’ ameanza kurejea katika ‘fomu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu, Risasi Jumatano l… Read More
HIVI NDIVYO ILIVYOKUA MAHAKAMANI KESI YA MADAWA YA KULEVYA INAYOMKABII CHID BENZ! Chid Benz (kushoto mwenye shati la bluu) akiingia katika lango la mahakama. ...Akiingia katika chumba cha kusikiliza kesi inayomkabili. ...Akitimu… Read More
HATARI SANA! MASTAA WAKIMBILIA KANISANI KUJISALIMISHA! Mc Pilipili.HUKU maajabu mengi yakiendelea kutokea kila kukicha na hivyo kuashiria mwisho wa dunia unakaribia, mastaa kibao wa filamu wameoneka… Read More
MISS TANZANIA MPYA LILIAN KAMAZIMA AFUNGUKA KUHUSU KUMRITHI SITTI MTEMVU! Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2… Read More
0 comments:
Post a Comment