KIKONGWE WA MIAKA 80 AWAKOMESHA MAJAMBAZI
Ajuza mwenye umri wa miaka 80 alimpiga mwizi usoni mwake nchini Uingereza na kumuogopesha kiasi cha kutoroka.
Mwanamke huyo, alikuwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Whitstable, Kent, wakati jambazi huyo alipomvamia. Alikuwa amevalia mavazi meusi yaliyokuwa yamefunuika kichwa chake.
Alipigana na jambazi huyo na kumgonga kinywani. Polisi mjini Kent wanasema kuwa wangali wanamsaka jambazi huyo.
Afisaa mkuu wa polisi katika eneo hilo alinukuliwa akisema:
Inaonekana mshukiwa huyo alimlenga mtu asiye wa kiwango chake.
Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa usiku Afisa mkuu wa polisi pia amewataka wakazi wa eneo hilo kutoa habari kuhusu tukio hilo.
je unamfahamu mtu yeyote ambaye alikuwa nje wakati wa usiku wakati ajuza huyo alipovamiwa na kurejea nyumbani akiwa na jereha kinywani? Tafadhali tunawaomba mtusaidie na uchunguzi wa kisa hiki
aliongeza kusema afisaa huyo.
0 comments:
Post a Comment