Monday 8 September 2014

STARS YAPIGWA 2-0 NA BURUNDI




Na Mwandishi Wetu, BUJUMBURA
TANZANIA imefungwa mabao 2-0 na Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa Uwanja wa Prince Louis Rwegasore mjini Bujumbura. 
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa Taifa Stars kutoka kwa Int’amba Murugamba, baada ya Aprili 26, mwaka huu kufungwa 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, siku ambayo kocha Mholanzi Mart Nooij alikuwa anawasili nchini kurithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen. 
Bao la kwanza la Burundi lilifungwa sekunde ya 40 tu, mfungaji Nahodha Said Ntibanzokiza aliyeunganisha kwa kichwa krosi muruwa na la pili dakika ya 24, mfungaji Ndikumana Yussuf aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Steve Ndikumasabo.Hiki kinakuwa kipigo cha tatu kwa Nooij katika mechi nane tangu aanze kuinoa Stars Aprili, awali akifungwa 4-2 na Botswana mjini Gaborone na 2-1 na Msumbiji mjini Maputo.

Mechi nyingine, Nooij ameipa ushindi mara mbili Stars 1-0 zote Dar es Salaam dhidi ya Malawi mchezo wa kirafiki na Zimbabwe kufuzu Mataifa ya Afrika.
Nooij pia ametoa sare mara tatu na Malawi 0-0 kirafiki mjini Mbeya, na Zimbabwe 2-2 Harare na Msumbiji 2-2 Dar es Salaam kufuzu AFCON.    
Vikosi vilivyoanza; Burundi; Mbonihankuy Innocent, Ntibanzonkiza Said, Kiza Fataki, Hakizimana Issa, Rachid Leo, Ndikumana Yussuf, Pierre Kwizera, Steve Ndikumasabo, Hussein Shaaban, Didier Kavumbangu na David Nshirimana.
Tanzania; Deo Munishi ‘Dida’, Said Mourad, Shomary Kapombe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Joram Mgeveke/Oscar Joshua, Erasto Nyoni/Himid Mao, Mrisho Ngassa/Simon Msuva, Mwinyi Kazimoto/Salum Abubakar 'Sure Boy', Mwagane Yeya/Juma Luizio, Amri Kiemba/Haroun Chanongo na Khamis Mcha ‘Vialli’.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA