Tuesday 23 September 2014

UKIWA HODARI WA KUHONGA, KAA MKAO WA KUACHWA WAKATI WOWOTE!



Leo nataka kuzungumzia suala la uhongaji katika uhusiano. Kuhonga ni tabia ambayo imeshamiri sana katika jamii yetu. Kipindi cha nyuma tumezoea kusikia ama kuona wanaume wakiwahonga wanawake lakini sasa hivi mambo yamebadilika.Wanawake nao
wameingia katika mkumbo wa kuwahonga wanaume ili wakubali kuwa nao kimapenzi tu ama waoane kabisa.Tabia hii imekuwa ikiwatia majaribuni walio wengi hali ambayo imesababisha baadhi ya watu wenye tamaa za kijinga kushawishika kufanya ngono na watu ambao katika mazingira ya kawaida wasingeweza kufanya nao.
Ni kitu cha kawaida kabisa kumkuta kijana wa kiume mwenye umri mdogo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama mtu mzima ambaye angeweza kuwa mama yake. Lakini hafanyi hivyo kwa matakwa yake bali kwa kushawishiwa na pesa ama vitu vingine vya thamani.
Kuna utata kidogo katika neno hili kuhonga, wapo wanaojiuliza kwamba hivi ninapompatia mpenzi wangu fedha kwa ajili ya matumizi madogomadogo nitakuwa nimemhonga? Katika uhalisia neno kuhonga ni kitendo cha mwanaume kutoa fedha ama zawadi kumpa mwanamke hasa pale anapomtongoza ili awe mpenzi wake ama mke wake.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA