VANESS MDEE AFUNGUKA KUHUSU KUTOKA KIMAPENZI NA JUX!
Vanessa Mdee aka Vee Money amekanusha tetesi zilizopo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Nitasubiri’ Jux.
Siku za hivi karibuni, Vanessa na Jux wamekuwa karibu kiasi cha watu kuhisi kuwa ni wapenzi.“Unajua labda watu hawafahamu tu lakini mie na Jux tumefahamiana muda sana na ni mtu ambaye huwa tunashauriana hasa mambo ya kazi zetu,” amesema Vanessa aliyecheka baada ya kuulizwa swali hilo.