Wednesday 30 November 2022

WANAWAKE, HAYA HAPA MAMBO 6 YATAKAYOFANYA UHUSIANO WAKO UWE IMARA ZAIDI



Habari yako msomaji wangu, nianze kwa kukushukuru sana kwa imani na heshima uliyonipa na unayoendelea kunipa katika kipindi chote cha mwaka huu wa 2022 na tunapoelekea mwishoni, nakutakia kila kheri na Mungu akakupe yale unliyomuomba na pia tukijaaliwa kuuvuka mwaka,2023 ukawe mwaka wa kupiga hatua za kusonga mbele.

Nimekuwa nikipata maswali mengi kwamba kwanini makala nyingi zimekuwa zikiwalenga wanawake ama mabinti na siyo wanaume huku wengine wakienda mbali zaidi na kusema kuwa wanaume ndio chanzo kikubwa cha mabalaa mengi katika mahusiano??

.... Kwanza nikiri kuwa kwa kuziweka kwenye mzani makala zinazowalenga wanawake ni nyingi zaidi ya zile zinazowalenga wanaume na sababu kubwa ni kwamba Mungu aliweka msingi wa mahusiano kwa wanawake kwa kuwa ndio watendaji wakuu wa mambo mengi hivyo nguvu waliyonayo wanawake katika mahusiano ni kubwa sana kulinganisha na ile ya wanaume (japo kuna mgawanyo wa majukumu) hivyo mwanamke imara ni mahusiano imara.

Leo nimeona niseme kwa ufupi na wanawake kuhusiana na mambo kadhaa amabayo yanaweza kuwa sehemu ya kuboresha afya ya mahusiano yao katika ngazi ya uchumba na hata ndoa.Nasema ni kwa ufupi kwani kila utakacho kisoma nitakiandika kwa mapana yake katika siku za usoni.

1. Muamini mmeo au mchumba wako.
Hapa sitaki kuweka maneno mengi, mfumo wa Maisha umewekwa katika hali ya usawa katika kupokea kwenye kile unachotoa. Wekeza Imani upate Imani wekeza Hofu na Hofu itakutawala daima.

2. Usikatishe tamaa katika maono yake.


Hapa ningependa utambue kuwa kusudi "kuu"la uumbaji wa mwanamke ni "usaidizi" kwa mwanaume..(nitalizungumzia kiundani katika makala maalum).ila  tambua kwamba utakapo kuwa msaada tosha na mwaminifu hadi mwenzi wako atakapotimiza malengo yake, ni dhahiri hata yale unayohitaji atakutimizia tena kwa moyo na bila ya kumuomba wala kumsukuma.


3. Usimlazimishe apende mambo unayoyapenda.
Ni vyema ukatambua kuwa kama binadamu tunavyotofautiana majina sura pamoja na tabia, haijalishi mahusiano yenu yamefika wapi hamuwezi kwa pamoja mkapenda kila jambo kwa usawa. Wewe hupendi mpira yeye anapenda mpira, yeye havutiwi na tamthiliya wewe unavutiwa sana na tamthiliya. Hapa haina haja ya kumlazimisha aje na awe na machaguo kama yako ,unaweza kumshawishi (kwa vitendo au kusifia na kuhusianisha na maisha yenu) na sio kumlazimisha. ::Wanaume hawapendi kulazimishwa kwani huona kana kwamba wanaburuzwa.



4. Usipange kumbadilisha.
 Hili nalo ni changamoto sana kwa wanawake wengi wanaoingia katika mahusiano, SAWA kila mtu huwa na maono ya mwenza anaedhani atamfaa au anaemuhitaji SIKATAI. Ila mpaka umeafiki kuingia nae katika mahusiano ni dhahiri ulijiridhisha kuwa mtaenda au pengine anakufaa, unapoingia kwenye mahusiano kwa lengo la kumbadilisha mtu kwanza kabisa unajiweka katika mazingira ya kuupoteza uhlisia wake ( na huenda mapenzi yakapungua) au ukashindwa kumbadilisha (ukabaki na hali ya kutoridhika) ndio maana huwa nashauri kwamba kabla ya kuanza mahusiano pima nyakati na umuombe Mungu kwa Imani yako ili akupe muongozo na majibu sahihi,kinyume na hapo hizi tunazoita heart-break zitakuwa wimbo wa kila kukicha.


5. Usidhani kwamba hawezi kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine.
Hapa sasa najua fika kuwa unahisi kama nakukosea heshima hivi (hahahaha) hapana ninamaanisha ninachosema. Zipo tafsiri nyingi za uzuri ila kwa ufupi twende tu na hio ambayo unayo katika mawazo yako kwa sasa. Ni kweli kamwe usidhani kwamba mwenza wako hawezi kukutana, kuona na kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine lakini kwa kutambua hilo nakupa kama changamoto USILEGEZE KAMBA. Kumekuwa na tabia kwa wanawake kuacha kujiweka sawa, kuonesha mapenzi na mahaba pale mahusiano yanapokolea ama pale mwanaume anapoanza kupunguza baadhi ya vitu, Hii sio sahihi.

Hebu tuutazame mfano huu amabao tunao katika maisha yetu ya kawaida . Tunazo chaneli kadhaa zinazoonesha vipindi vya televisheni lakini hata wewe ipo ile ambayo lazima uitazame mara kwa mara kwakuwa inakuvutia aidha kwa mpangilio wa vipindi au aina ya uwasilishaji LAKINI hii haimaanishi kuwa chaneli ambazo huwa hauzipi kipaumbele kuwa ni mbaya na haizifai kutazamwa. 

Siku chaneli unayopendelea ikianza kupunguza baadhi ya mambo yaliyokufanya uvutike ni dhahiri utavutika kuanglia na kwingine kuna vipindi vya aina gani na kwakulitambua hilo kiushindani chaneli hizi huweka bidii kila iitwapo leo kuhakikisha inaboresha zaidi na zaidi...Je upo tayari kulegeza kwakuwa amekuchagua wewe????


6. Usilazimishe kuwajibika juu ya mambo yako: Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa anafanyiwa hivyo na wewe unataka, ladies hicho sio kipimo cha mapenzi.

Kdmula anasema: Kama upo kwenye uhusiano ambao hauna uhakika nao ni dhahiri Mungu hakuwa sehemu ya kuanzishwa kwake na pengine huyo siyo sahihi kwako. Haujachelewa lakini usiwe mtu wa kurudia makosa mara kwa mara kwa kushindwa kuzihimili hisia na tamaa za mwili.
Hebu weka nia sasa kwamba 2023 NI MWAKA WAKO hakuna kulia tena na mahusiano yako yatakuwa na ustawi bora utakaokupa zawadi ya agano la ndoa.(Kama lengo sio Ndoa ,basi ni vyema ukajiondoa)


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA