Friday, 12 September 2014

YULE JAMAA WA MENO YA CHUMA ALIYEIGIZA SINEMA ZA BOND AFARIKI DUNIA


MUIGIZAJI Richard Kiel  ambaye alicheza kama Jaw katika sinema mbili za James Bond amekufa mjini california akiwa na umri wa miaka 74.

Muigizaji huyoa mbaye alikuwa na urefu wa kuchusha na kuigiza katika sinema The Spy Who Loved Me  ya mwaka 1977 na Moonraker ya mwaka 1979,amekufa akiuwa hospitalini Fresno jana, Jumatano.

Msemaji wa Saint Agnes Medical Center alithibitisha kifo cha Kiel lakini hakusema sababu ya kifo chake.

Muyigizaji huyo ambaye alikuwa na urefu wa futi 7 na inchi 2  pia alishawahi kucheza komedi ya michezo ya  Happy Gilmore ya mwaka 1996, ambayo kinara wake alikuwa Adam Sandler.

Kiel alipata nafasi ya kuigiza katika sinema kwenye miaka 1950s lakini akachanua zaidi wakati alipoigiza adui wa Bond akiwa na meno ya chuma. 

Akiwa amezaliwa Detroit, Michigan, Kiel alikuwa na tatizo la homoni ambalo inadaiwa liliongeza urefu wake.

Sinema yake ya kwanza iliyomtoa ilikuwa ni ya mwaka 1959 alipocheza kama kiumbe wa ajabu  kwa jina la Kanamit katika sinema ya Twilight Zone.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA