AIBU: WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAKAMATWA WAKILIMA SHAMBA WAKIWA UCHI
09:11 |
No Comments |
Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watu wanne wa familia
moja kwa tuhuma ya kukutwa wakilima uchi wa mnyama shambani kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu Venansi Kimario
alisema tukio hilo limetokea septemba 2 majira ya saa 12 asubuhi
katika kijiji cha Bushikwamala kata ya Kalemela wilayani Busega Mkoani
Simiyu
Kimario alisema kuwa watu hao walikamatwa na jeshi la polisi alfajiri
huko Bushigwamhala wakiwa wanalima kwenye shamba lao na walipohojiwa
walidai kuwa walielekezwa na babu yao kipindi cha uhai wake kuwa
wakilima uchi watapata mavuno mengi.
Kamanda Kimario aliwataja waliokamatwa kuwa ni Makoye Kagoje (42), na mke
wake Neema Kigwela (31) pamoja na watoto wao, mmoja wa kiume (15) na
wa kike (12) majina yamehifadhiwa.
Aidha Kimario alisema watu hao pamoja na watoto wao wanashikiliwa na
jeshi la polisi kwa kukutwa wakifanya vitendo vya ushirikina.
Babu yao alishafariki mwaka jana na aliwaambia kuwa wakilima wapo uchi
watapata mavuno mengi, hivyo waliamua kufanya hivyo kutokana na wosia
wa babu yao
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema
liliweza kufika katika eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa
wanaendelea kulima bila nguo.
Hata hivyo Kimario amewataka watu wasijishirikishe kwenye
vitendo vya ushirikina na siyo kwamba ukilima uchi utapata mazao mengi
tofauti na kufuata kanuni za kilimo bora, viongozi wa madhehebu ya
dini na viongozi wa serikali tuwaelimishe watu waachane na imani za
kishikina .
EDDY BLOG
Na Faustine Fabian-Simiyu
Related Posts:
KURASA ZA MAGAZETI LEO WEDNESDAY /JUMATANO 30/7/2014 BOFYA HAPA KUYASOMA YOTE>> Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to… Read More
MWANAMKE ALIEPANGA KUMUUA MUMEWE AENDELEA KUSOTA RUMANDE:ARUSHA MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha jana imekataa ombi la hati ya dharura ya dhamana ya mke wa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Janeth Ja… Read More
KURASA ZA MAGAZETI YA BONGO LEO TUESDAY /JUMANNE 29/7/2014 Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook … Read More
MAAJABU: PICHA AMBAZO INAKUBIDI UZITAZAME KWA MAKINI ILI UZIELEWE!!!! KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA … Read More
MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAN UTD JI SUNG PARK AFUNGA NDOA Maharusi – Park na Kim Ji-Sung Park ambae ni nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Korea ya Kusini amefunga ndoa na mchumba wake wa siku ny… Read More
0 comments:
Post a Comment