BABA MZAZI ADAIWA KUMCHINJA MWANAYE SENGEREMA MWANZA
11:30 |
Baba mzazi mkazi wa Sengerema anadaiwa kumuua mwanaye wa miaka minne kwa kumchinja koromeo na kumchoma kwa kisu kwenye kitovu na utumbo kutoka nje.
Mzazi huyo anadaiwa kufanya mauaji hayo juzi alfajiri baada ya kumchinja aliuchoma kwa kisu mwili wa mtoto huyo sehemu mbalimbali ikiwemo masikioni na kifuani.
Gazeti la MWANANCHI ambalo lilikua shuhuda limedai baada ya kufanya kitendo hicho alianza kufukuza wananchi waliokusanyika eneo hilo kwa kuwatishia kuwachoma na kisu.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alizidiwa nguvu na wananchi na kuanza kumshambuliwa kwa kipigo hadi alipookolewa na Mwenyekiti wa mtaa.
Mama mzazi wa watoto hao alisema kabla ya kutengana na mumewe huyo alizaa nae watoto watatu na kwamba ameshangazwa kupata taarifa za mwanaye kuuawa na baba yake.
Jeshi la Polisi linamshikilia kwa uchunguzi huku likisubiri taarifa ya hospitali kuhusu utimamu wa akili yake.
-MWANANCHI@VIA EDDY
Related Posts:
TWIGA KUCHEZA NA MALAWI NOVEMBA 7 Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi No… Read More
MKWASA AITA 28 STARS KUIVAA ALGERIA Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikos… Read More
MAWAZIRI 5 WAANGUSHWA UCHAGUZINI TANZANIA Makao makuu ya matokeo ya uchaguzi nchini Tanzania Mwaziri watano wa serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,… Read More
JE, UNATAMBUA MAMBO AMBAYO UKIYAFANYA UNASABABISHA MAISHA YAKO KUWA MAGUMU KULIKO INAVYOTAKIWA? SOMA UJIELIEMISHE Kuna msemo aliwahi kuusema OScar Wilde na katika lugha yake unasomeka hivi; nanukuu, Life is not complex. We are complex. Life is simple,and th… Read More
MATOKEO RASMI YA WAGOMBEA URAIS MAJIMBO 26 U … Read More