Saturday, 29 October 2016

MO, KICHUYA WAZIDI KUNOGA SIMBA IKIENDELEZA WIMBI LA USHINDI KWA KUIFUNGA MWADUI 3 - 0

Kichuya, Photo credit Bin Zubery Blog

KIUNGO Mohamed Ibrahim 'MO' ameonyesha  kiwango cha hali ya juu Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage.Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0, yote yakifungwa na viungo wapya waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar.

Pamoja na ushindi huo wa mabao 3 mawili yakifungwa na Mohamed Ibrahim pamoja na Shiza Kichuya  bado Simba waliendelea kucheza vizuri huku wakionekana kama wapo nyumbani baada ya kutawala sana mchezo huo hasa kipindi cha pili ambapo Mwadui hawakuwa mchezoni na endapo Wekundu hao wangeongeza umakini wangepata mabao mengi zaidi.


Simba wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 32 baada ya kushuka dimbani mara 12 huku wakioneka wana dhamira ya kweli ya kunyakua ubingwa msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA