LAANA::IMAM SHOGA AWAFUNGISHA NDOA WANAWAKE WA-IRAN NCHINI SWEDEN
Maryam Iranfar (kushoto) akimbusu mkewake, Sahar Mosleh.
Maryam Iranfar, Sahar Mosleh wakiwa na nyuso za furaha baada ya harusi.
Imam Zahed (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wapenzi hao baada ya kuwafungisha ndoa.
WAKIWA nyuso za furaha, wanawake wawili, wananchi wa Iran, Sahar Mosleh na Maryam Iranfar hatimaye walifunga ndoa huko Stockholm, Sweden, kama mume na mke baada ya miaka tisa ya kuishi pamoja.
Wawili hao waliikimbia nchi yao ya Iran ambayo ina sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Ukiachana na umbali wa kutoka kwao hadi Sweden, madada hawa waliokutana kwenye mtandao walikuwa huru kufurahia siku yao hiyo kubwa huko Sweden ambapo harusi ilifanyika.
Maryam Iranfar ambaye ndiye mwanamme anatarajiwa kupata mtoto na Sahar Mosleh (mkewe) ambaye ana ulemavu wa mifupa, walifungishwa harusi na Iman Ludovid Mohamed Zahed ambaye pia ana mahusiano ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Imam huyo anayeishi Afrika Kusini na ambaye ni raia wa Algeria anayefahamika sana katika jamii ya mashoga na wasagaji katika nchi za Kiislamu, alisema amefurahi kuona wanaharusi hao wakiwa na furaha na kufanya jambo zuri la kuamua kuishi maisha huru katika nchi za watu.
“Nashukuru kwa harusi nzuri kama hii iliyoniwezesha kuwabariki wanandoa hawa, ” alisema Imam huyo.
Kama wangekuwa nchini kwao Iran ambayo ina sheria ya kupigwa bakora hamsini mara tatu kila wanapokutwa na mahusiano hayo, na ambapo mara ya nne huwa ni adhabu ya kifo, wanadada hawa wasingewezeshwa kufunga harusi hiyo.
“Nimefurahi pia kuona wanadada hawa wameanzisha familia yao baada ya miaka mingi ya mateso kwani ni vigumu kusafiri umbali mrefu kutoka nyumbani na kuja nchi za watu na kuanza maisha kwa pamoja,” alisisitiza imam huyo