Friday 24 October 2014

TAARIFA KUHUSU! CHIDI BENZ KUKAMATWA NA POLISI AIRPORT AKIDAIWA KUKUTWA NA MADAWA



Najua kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid Benz amekamatwa na Polisi.
Taarifa zinasema kakamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea 


Mbeya na hiyo imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni kosa kwa yeyote kukutwa navyo.
Wakati mwandishi wa habari hizi akiendelea kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi, tumezungumza na muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz ndio alikua anakwenda kushiriki kesho.

Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu &“Sijapewa taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba haviruhusiwi kupita Airport“
Chidi Benz alikua ameongozana na msanii mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi kabaki na Polisi na Shetta amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea Mbeya.


Tunaendelea kufatilia zaidi hizi taarifa ili kupata uhakika kutoka kwa upande wa Polisi.
-DJ SEK

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA