Friday, 7 November 2014

FORBES WATOA MAJINA YA WASANII WA KIKE WALIOINGIZA MKWANJA MREFU ZAIDI MWAKA HUU, NICKI MINAJ TUPA KULE. HUYU NDO KAWA NAMBA 1

beyonce
Forbes wametoa majina ya wasanii wanaopokea mkwanja mrefu zaidi huko Marekani, list hiyo imeshikiliwa na wadada wanaofanya vizuri kwa sasa huku pia wakiwemo waliotamba miaka hiyo kama Celine Dion. Katika list hiyo anayeongoza ni Beyonce ambae ameweza kuingiza dola za kimarekani milion 115 hii ni ongezeko mara mbili zaidi ya pesa aliyoingiza mwaka jana. Mwaka jana aliingiza dola za kimarekani Millioni 53. Beyonce ameingiza mkwanja huo kupitia show anazofanya na mauzo ya kazi zake.
Katika list hiyo wasanii kama Madonna, Alicia Keys, Nicki Minaj, Miranda Lambert naShania Twain hawajaingia kutokana na mapato yao kushuka mwaka huu. Unaweza icheki list na mkwanja wanaoingiza wasanii hao hapa chini…

1. Beyonce – $115million
2. Taylor Swift – $64 million
3. Pink – $52million
4. Rihanna ($48 million)
5. Katy Perry ($40 million)
6. Jennifer Lopez ($37 million)
7. Miley Cyrus ($36 million, tie)
7. Celine Dion ($36 million, tie)
9. Lady Gaga ($33 million)
10. Britney Spears ($20 million)
-B.CLAN

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA