HATARI SANA! MASTAA WAKIMBILIA KANISANI KUJISALIMISHA!
Mc Pilipili.HUKU maajabu mengi yakiendelea kutokea kila kukicha na hivyo kuashiria mwisho wa dunia unakaribia, mastaa kibao wa filamu wameonekana kujisalimisha kanisani na kuhudhuria ibada ya kiroho ya Inuka Uangaze maeneo ya Vatican -Sinza jijini Dar es Salaam.Chanzo makini kilicho ndani ya kanisa hilo kilisema kwamba wasanii wengi wamevutiwa na huduma hiyo ambayo maombi yake hufanyika kila Jumanne na Jumatano na huongozwa na mchungaji mkuu, Buldoza Mwamposa.
Hosti wa kipindi cha 'Wanawake Live' cha chaneli Five, Joyce Kiria Baadhi ya wanaotajwa kuonekana kanisani hapo ni pamoja na Dotnata, Thea, Mainda, Mc Pilipili, Joyce Kiria na Dokii. Msemaji wa mchungaji Mwamposa aliyejitambulisha kwa jina la Leonard Mwazembe alikiri nyota hao kupata maombi kanisani kwake.