Friday, 18 March 2022

CATC YAENDELEA KUNOA WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA

 


Mkurugenzi wa Rasilimali watu na huduma wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Teophory Mbilinyi akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Uongozaji Ndege kwa kutumia rada, Ufundi wa Mkanda wa kupokea Mizigo katika Viwanja vya ndege pamoja na Usalama katika Viwanja vya ndege   yanayotolewa na  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).




Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambaye ni Mgeni Rasmi, Bw. Hamisi Amiri akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Uongozaji Ndege kwa kutumia rada, Ufundi wa Mkanda wa kupokea Mizigo katika Viwanja vya ndege pamoja na Usalama katika Viwanja vya ndege   yanayotolewa na  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).



Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), John Ndimbo akizungumzia namna walivyoendesha mafunzo hayo kwa ufanisi na kwa kuzingatia ubora kimataifa. 


Mtaalam wa Uundaji wa mitaala na mafunzo kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) Bw. Simon Lugaba akielezea hatua walizopitia katika kuusuka mtaala ambao licha ya kwamba utatumika kufundisha wataalam utauzwa kwa vyuo vingine na kuingizia kipato CATC.


Baadhi ya wahitimu wa kozi ya Uongozaji Ndege kwa kutumia rada wakifuatilia hotuba katika mahafali chuoni hapo.


Wahitimu wakifuatilia yanayoendelea



Kwa niaba ya wahitimu wote Bw. Godlove Longole ambaye ni muongozaji ndege muandamizi akiushukuru Uongozi wa Chuo kwa namna ilivyoaandaa na kuwasilisha mafunzo hayo kwao.


Picha za pamoja






0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA