"NILIACHA KAZI ILI KUFUATA KIPAJI CHANGU " MC PILI PILI AFUNGUKA
Alizaliwa tarehe 1 Oktoba 1985 wengi
wanamfahamu zaidi kama Mc Pili Pili lakini jina lake halisi ni Emanuel Mathias
mchekeshaji na mshereheshaji anayefanya vizuri katika tansia ya komedi nchini
Tanzania.
Katika mahojiano maalum na
Funguka Live Blog Mc pili pili alieleza kuwa aliamua kufanya maamuzi magumu ya
kuachana taaluma yake ya ualimu alipokuwa akifundisha shule ya Dct Jubilee High
School mjini Dodoma na kuelekea jijini Dar es salaam…. “Nilikuwa mwalimu wa
sekondari kwa miaka sita (6) nikaamua kuacha na kuhama toka Dodoma kuja Dar es
salaam,niliamua kufuata kipaji changu”
Mc pili pili akifanya mambo katika moja ya show zake |
“Kwa muda wa miaka kumi na tano
nimekuwa mshereheshaji na mchekeshaji ila katika miaka mitano ya karibuni ndio
nimekuwa serious kwenye komedi”.Pili pili aliongeza kwa kuwataja wale
waliomuhamasisha na kumpa ari ya kuanza kufanya komedy kama kazi, “kwa hapa
nyumbani naweza kusema ni Joti,Masanja pamoja na marehemu Sharo millionea
lakini kwa Afrika mashariki ni Eric Omondi na Afrika kwa ujumla siwezi kuacha
kuwataja Basket Mouth na Trevoh Noah ila nje ya Afrika Kevin Hart amekuwa role
model wangu”…
Mc pili pili akiwa na Joti |
Mc pili pili ambaye pia ni mtangazaji wa redio Times Fm na mkurugenzi
wa Pili pili events alikiri kuwa kwa
sasa aina ya komedi anayofanya “stand up comedy” ile ya kwenye majukwaa bado
haijapata muitikio mkubwa hapa nchini kama ilivyo kwa majirani zetu wa Kenya na
Uganda. “Kikubwa ni kuitambulisha zaidi na zaidi nitapeform Dar es salaam,Arusha ,Dodoma na
Mwanza mwaka huu ila pia nina mpango wa
kuperform nchini Marekani na U.K kwa
Watanzania waishio huko nadhani kwa nguvu hii “stand up comedy” itapata
kukubalika zaidi na zaidi”.
Funguka live Blog ilipotaka kujua kama
Mc pili pili anampango wa kufanya falimu alisema kuwa kwa sasa bado hajaamua
ila baadae anaweza akaingia katika kucheza filamu kwa sasa naweka videos za kazi yangu Youtube na kwa kweli zinafanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment