Sunday 5 April 2015

CHARLES HILLARY NKWANGA AAGA RASMI BBC, KURUDI AZAM TV

Mtangazaji Charles Hillary (kulia) akiwa na mtangazaji mwanzake wa BBC wakati alipokuwa akiaga rasmi kituoni hapo.
Mmoja kati ya wafanya kazi wenzake akionesha jezi iliyoandikwa jina la Nkwanga.
KAMA BADO HUJADOWNLOAD ANDROID APPLICATION YA BLOG HII BOFYA HAPA UWEZE KUPATA HABARI ZETU MOJA KWA MOJA   
Charles Hillary akiwa mtangazaji mwenzake wa BBC Zuhura Yunus katika picha ya pamoja.
Charles Hillary akiwa amevaa jezi hiyo.
Aliyekuwa Mtangazaji wa BBC Charles Hillary ameaga rasmi jana kwenye kituo hicho na hivi punde atarudi nchini Tanzania kufanya kazi yake katika kituo cha Television cha Azam TV.
Katika tasnia ya habari, Charles Hillary amefanya kazi ya utangazaji kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1993 akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam. Mwaka 1994 alijiunga na Radio One ikiwa ni radio ya kwanza binafsi kuanzishwa nchini Tanzania.

BOFYA HAPA KUIFAHAMU HISTORIA YA PASAKA

Mwaka 2003 aliamua kuacha kazi Radio One na kujiunga na Radio DW Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ambapo alifanya kazi mjini Koln na baadae Bonn hadi mwaka 2006 alipokatiza mkataba wake baada ya kupata ajira Idhaa ya Kiswahili ya BBC London ambako alijiunga tarehe Aprili 14, 2006.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary. Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alithibitisha Hillary kutarajiwa kujiunga na Azam Media akiwa na historia nzuri kwenye vyombo vya habari kuanzia alipoanza kazi hiyo.
Jana Charles Hilary ameaga rasmi katika kituo cha utangazaji cha BBC na kuahidi kulitumikia taifa lake tena akiwa Azam TV.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA