Sunday, 26 April 2015

KILIMANJARO..FUSO YAACHA NJIA YATUMBUKIA MTARONI NA KUMJERUHI MPITA NJIA


Na Dickson Mulashani

Muda mfupi uliopita gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 167 CLV mali ya kampuni ya MACHAVA mkoani Kilimanjaro limeacha njia na kutumbukia katika mtaro katika barabara iendayo katika kiwanda cha sukari TPC nje ya machinjio ya mkoa.

Wakizungumzia ajali hiyo ambayo ilisababisha jeraha dogo katika mguu wa mpita njia, mashuhuda walieleza kuwa mwendo kasi na ufinyu wa barabara ndio chanzo cha ajali hio.
Vile vile wapo waliomtuhumu dereva kuwa alikosa umakini kwakuwa alikuwa amepakia abiria mwanamke ,tuhuma ambazo FUNGUKA LIVE haikuweza kizithibithisha kwani wakati mwandishi alipofika katika eneo la tukio dereva wa gari hilo alikwisha toweka katika eneo la tukio.



FUNGUKA LIVE inawaasa madereva kuwa makini pindi waeneshapo magari,vile vile inashauri ujenzi wa bara bara uwe mpana kuepusha lawama kwa watumiaji.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA