Showing posts with label ajali. Show all posts
Showing posts with label ajali. Show all posts

Friday, 12 May 2017

HALI ILIVYOKUWA BAADA YA MAPOROMOKO YA MAWE TANGA

Jeshi la Polisi mkoani Tanga jana  lilifunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba  alisema, maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini.

"Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo.

"Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict.

Kwa upande mwingine Kamishna huyo alisema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri.

Wednesday, 11 January 2017

12 WAPOTEZA MAISHA AJALI YA BOTI BAHARI YA HINDI ,25 WANUSURIKA

Image result for AJALI YA BOTI
Picha toka Maktaba

Ajali ya Jahazi ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria 12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.

Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe, chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi na kuzama

Akizungumzia tukio hilo,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.

Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko ambayo yanafanyika leo  na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.

Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

“Ajali sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.

Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.

Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.

Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.

Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huku watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu mengine.

Wednesday, 30 November 2016

MATUKIO KATIKA PICHA KUHUSU AJALI YA NDEGE ILIYOUWA WACHEZAJI WA BRAZIL

Mabaki ya ndege namba CP 2933 iliyoanguka katika jimbo la Medellin nchini Colombia huku ikisemekana kuwa watu 75 wamepoteza maisha wakiwemo wachezaji wa timu ya Chapecoense ya nchini Brazil


 Kikosi cha waokoaji kikiendelea na zoezi la kutoa miili ya watu walioaga dunia katika ajali hiyo


 Mashabiki wa Chapecoense wakiwa wamejikusanya kwenye makao makuu ya klabu hiyo maeneo ya Chapeco nchini Brazil


 Waokoaji wakiwa wamebeba moja ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo


Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea huku taarifa zikisema ni watu sita pekee ndio waliotoka wakiwa hai


 Waokoaji wakipanga miili ya baadhi ya abiria waliofariki 


 Hii ndio ndege iliyopata ajali


 Mchoro ukionyesha safari ya ndege hiyo kabla haijapata ajali 


 Mchezaji Jackson Follmann ametajwa kuwa ni kati ya watu sita walionusurika katika ajali hiyo


 Kikosi cha Chapecoense


 Hapa viongozi na wachezaji wa timu hiyo wakiwa ndani ya ndege kabla hawajaanza safari iliyokatisha uhai wao


Beki wa timu hiyo Alan Rushel aliposti video kwenye mtandao wa Instagram akiwa na kipa Danilo kabla ndege haijaondoka nchini Brazil


 Rushel alikuwa wa kwanza kukimbizwa hospitali kupata matibabu huku akiwaasa madaktari kuwa makini na pete yake ya ndoa isijepotea


 Kikosi cha huduma ya kwanza kikiwa jirani na eneo la tukio


 Meya wa jiji la Medellin, Fico Gutierrez akiwasili katika eneo la tukio


Madaktari na wauguzi wakisubiri majeruhi ili kuwahudumia


Rushel na Danilo wanatajwa kuwa ni kati ya abiria sita waliotoka wakiwa hai


 Nembo ya klabu hiyo iliyookotwa baada ya ajali hiyo


 Ndege hiyo iligawanyika vipande viwili baada ya kuanguka


 Madaktari wakijitahidi kuokoa uhai wa mmoja wa abiria wa ndege hiyo





Simanzi kubwa.....wachezaji watatu ambao hawakusafiri na timu wakiwa na huzuni kubwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha timu hiyo


Ndugu, jamaa na marafiki wakisubiri taarifa kutoka eneo ilikotokea ajali

Tuesday, 29 November 2016

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA TIMU YA SOKA CHAPECOENSE YA BRAZIL YAANGUKA LEO ASUBUHI NCHINI COLOMBIA

Mabaki ya ndege
Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.


Maafisa wanasema watu sita wamenusurika. huku chanzo cha kuanguka  Ndege hiyo kikielezwa ni kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme huku taarifa zikisema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.

Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".
Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, amesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura huku hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.
Sambamba na hilo hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura.

Friday, 30 September 2016

TRENI YAGONGA STESHENI NA KUUA MTU MMOJA NA KUJERUHI WENGI MAREKANI

Mtu mmoja ameripotiwa kufa na makumi kujeruhiwa, baadhi yao vibaya mno baada ya treni kugonga stesheni katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Treni hiyo imeripotiwa kugonga kizuizi cha eneo la tiketi na kuingia katika eneo la mapokezi la stesheni ya Hoboken.
   Watu waliojeruhiwa wakiwa wamelazwa kwenye machela maalum za magari ya wagonjwa
             Mwanamke aliyejeruhiwa akiwa amewekewa kifaa maalum cha hewa ya oxygen
                    Waokoaji wakiangalia ndani ya treni kuangalia kama kuna watu waliojeruhiwa 

Sunday, 31 July 2016

WATU 16 WAFARIKI BAADA YA PUTO LA KUPAA ANGANI KUWAKA MOTO


Watu wapatao 16 wamekufa baada ya puto la kuruka kwa kutumia joto kupata moto likiwa angani na kuanguka kisha kuuwa watu wote waliokuwamo nchini Marekani.

Moto huo unaaminika ulitokea katika eneo la kikabu cha kusimamia watu wakati safari hiyo ya anga ikiwa kati kati, na kisha kuanguka chini huko Lockhart maili 30 kutoka Austin.

Mkuu wa polisi wa Kaunti ya Caldwell, ameviambia vyombo vya habari kuwa hakuna mtu aliyenusurika.  

Thursday, 7 July 2016

IDADI YA WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA CITY BOY WAFIKIA 32

Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya Kampuni ya City Boy imeongezeka na kufikia 32 baada majeruhi aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) kufariki dunia.

Ajali hiyo iliyohusisha mabasi hayo wakati moja likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyangana lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam, ilitokea saa tisa Jumatatu katika eneo la Maweni, Kata ya Kintiku Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza jana Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,  Dk Ibehzi Ernest alisema kazi ya kutambua miili ya marehemu hao bado inaendelea.

Alisema hadi jana miili ya watu 25 waliokufa kwenye ajali hiyo ilikuwa imetambuliwa na ndugu zao. Dk Ernest ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Ajali, Upasuaji na Mifupa alisema kati ya maiti 25 zilizotambuliwa 12 zimechukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

“Wengine wametibiwa na kuruhusiwa tumebaki na majeruhi watano ambao hali zao zinaendelea vizuri,” alisema. 

Kwa siku nzima ya juzi na jana watu walikuwa wakipishana kuwatambua ndugu zao katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Dodoma. Kutokana na miili kuharibika, ndugu hao walikuwa wakirudi mara mbili kuangalia. 

Saturday, 21 May 2016

JESHI LA MISRI LATOA PICHA ZA MABAKI YA NDEGE YA EGYPTAIR


Jeshi la Misri limetoa picha za vitu vilivyopatikana katika zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la EgyptAir iliyotoweka katika eneo la bahari ya Mediterranea.

Picha hizo zinaonyesha vitu kama jaketi la kujiokolea, sehemu za viti na vitu vingine mbalimbali vinavyoonyesha ni vya ndege hiyo aina ia Airbus.
Ndege hiyo ilitoweka Alhamisi ikiwa angani ikitokea Jijini Paris kwenda Cairo ikiwa na abiria 66 pamoja na wahudumu.
                               Jaketi la kujiokolea maisha mtu akiwa majini la ndege hiyo
               Sehemu ya mabaki ya viti vya ndege kama inavyoonekana kwenye picha hii

Wednesday, 13 January 2016

TAKWIMU:::WATU 331 WAFARIKI DUNIA MKOANI MBEYA KWA AJALI ZA BARABARANI 2015


Ajali
Jumla ya watu 331 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani mkoani Mbeya katika kipindi cha mwaka 2015 ikiwa ni ongezeka la vifo 27 ikilinganishwa na vifo 304 vilivyotokea mwaka 2014.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Ahmed Msangi amesema ongezeko hilo la vifo linaenda sambamba na ongezeko la makosa ya usalama barabarani na idadi ya wahalifu wa makosa hayo.
ajali 2
Katika mahojiano maalumu na Kituo Star TV, Kamanda Msangi amesema mwaka 2014 jumla ya makosa 61,466 yamepatikana wakati mwaka jana makosa yalikuwa 76,346 ikiwa ni ongezeko la makosa 14,898 ambapo kati yake mwaka 2015 makosa 71, 429 na 54,849 ya mwaka 2014 kwa pamoja yametozwa adhabu zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3 na Milioni 203 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Milioni 497.4 kwa tozo za mwaka 2014.
Kuhusu Pikipiki za miguu miwili na mitatu maarufu kama na Bajaji, Kamanda Msangi amesema ajali zake nazo zimeongezeka kutoka 141 mwaka 2014 mpaka 159 mwaka jana ambazo kwa pamoja zimesababisha vifo 162 na kujeruhi watu 231 na kwamba nyingi zimesababishwa na uzembe wa kukosa umakini kwa madereva.
Jiji la Mbeya lina pikipiki za miguu mitatu zaidi ya 2100 wakati pikipiki za miguu miwili ni zaidi ya 3000.GPL

Sunday, 1 November 2015

NDEGE YA URUSI YAANGUKA IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200





JamaaImage copyrightAP
Image caption
Jamaa na marafiki wamefika uwanja wa ndege wa St Petersburg kutafuta habari kuhusu wapendwa wao

Watu 224 wamefariki baada ya ndege ya shirika moja la Urusi kuanguka katika eneo la Sinai nchini Misri.
Ndege hiyo aina ya Airbus A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa St Petersburg nchini Urusi ilipoanguka.
Maafisa wa serikali wa Misri wamenukuliwa na shirika la habari la AP wakisema hakuna manusura wowote waliopatikana.
Maafisa wa usalama eneo hilo wameambia shirika la habari la Reuters kwamba kufikia sasa miili 150 imepatikana.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma risala za rambirambi kwa jamaa za waathiriwa na kuagiza uchunguzi ufanywe.
Ujumbe kutoka Urusi ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi Maksim Sokolov umeelekea eneo la mkasa huku Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi naye akirejea nyumbani kutoka Bahrain.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, baadhi ya ripoti zikisema ilitoweka karibu na visiwa vya Cyprus. Lakini afisi ya Waziri Mkuu wa Misri Sharif Ismail imethibitisha kwamba ndege hiyo ilianguka katikati mwa eneo la Sinai.
Afisi hiyo imeongeza kuwa Bw Ismail ameunda kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
Wengi wa abiria walio kwenye ndege hiyo ni watalii kutoka Urusi.
Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Kogalymavia. Ripoti za karibuni zinasema ilikuwa imewabeba abiria 217 na wahudumu saba.



Shirika la Urusi linalosimamia safari za ndege Rosaviatsiya limesema ndege hiyo safari nambari 7K 9268 iliondoka Sharm el-Sheikh saa 06:51 saa za Moscow (0:351 GMT) na ilitarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Pulkovo mjini St Petersburg saa 12:10.
Waliongeza kuwa ndege hiyo ilikosa kuwasiliana na wasimamizi wa safari za ndege Cyprus dakika 23 baada ya kupaa kama ilivyoratibiwa na ikatoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Ubalozi wa Urusi nchini Misri umesema ndege hiyo ilijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa El Arish.
Kituo maalum kmefunguliwa uwanja wa ndege wa Pulkovo kusaidia jamaa za abiria waliokuwa kwnnye ndege hiyo, shirika la habari la Tass limesema likinukuu maafisa wa jiji la St Petersburg.
Kundi la Kiislamu la Islamic State (IS) limedai kuhusika kuangusha ndege hiyo. Eneo ambalo ndege hiyo ilianguka limekumbwa na maasi ya kundi la Sinai Province ambalo lina ushirika na kundi la IS.
Maafisa wa usalama Misri hata hivyo walikuwa awali wamesema ajali hiyo ilisababishwa na hitilafu za kiufundi na kwamba ni vigumu kwa waasi hao kwa kutumia makombora.
-BBC

Tuesday, 16 June 2015

TASWIRA YA AJALI YA COASTER ILIYOGONGANA NA LORI NA KUUA WATU 23 IRINGA

Coaster la Kampuni ya Another G baada ya ajali.
Taswira kutoka eneo la ajali hiyo.
WATU zaidi ya 23 wamepoteza maisha katika ajali ya gari aina ya Coaster mali ya Kampuni ya Another G inayofanya safari zake kati ya Njombe - Iringa baada ya kugongana na lori jana usiku.
Ajali hiyo imetokea eneo la Kinyanambo nje kidogo na mji wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati Coaster hiyo ikitokea mkoani Iringa kwenda Njombe.
-GPL

KWA HALI HII AJALI ZITAKWISHA KWELI?

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA