Friday 10 April 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.

KAMA BADO HUJADOWNLOAD ANDROID APPLICATION YA BLOG HII BOFYA HAPA UWEZE KUPATA HABARI ZETU MOJA KWA MOJA   AU WASILIANA NASI KUPITIA 0652 571233

Jeshi la Polisi nchini linawataka wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi haraka.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika. Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA