Wednesday 14 September 2016

UEFA:::ARSENAL YAIKOMALIA PSG UGENINI

 Alexis Sanchez akijipinda na kuachia shuti lililosawazisha goli 
Alexis Sanchez ameisaidia Arsenal kuambulia pointi moja katika Ligi ya Mabingwa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo dhidi ya Paris St-Germain.

Edinson Cavani aliipatia goli la kuongoza PSG baada ya sekunde 42 tu na angeweza kuwa amefunga magoli matatu kabla ya mapumziko lakini alikosa magoli mengine mawili.

Alex Iwobi almanusura aipatie Arsenal goli la ushindi la dakika za mwisho kabla ya Olivier Giroud na mchezaji wa PSG, Marco Verratti kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
                            Mpira wa kichwa uliopigwa na Edinson Cavani ukiingia wavuni 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA