Tuesday 10 May 2016

ELIMU !! JINSI YA KUTUNZA MAZINGIRA YETU





 Magonjwa mbali mbali yatokanayo na mzagao wa takataka katika mazingira ya jiji la Dar es Salaam ni tishio kwa walio wengi hasa wakazi wa maeneo yanayohusiana na biashara za vyakula na maji ukiachilia mbali  matunda  ambayo  wengi huyatumia bila kujua kuwa yapo katika hali gani za usalama kwa afya zao.
Matunda hayo yanayouzwa na wenzetu katika kujitafutia riziki zao za kila siku ni chanzo cha kuibuka kwa magonjwa yanayowasumbua wenzetu katika hospitali nyingi, hasa magonjwa ya tumbo ambayo wengi wetu wakiugua hawafanyi kingine ila kununua dawa katika maduka ya dawa yaliyo karibu na makazi yao na kukuta wakati mwingine wanajiongezea matatizo ya afya zao bila kujua kile wanachoki fanya kwa dhana kwamba wanajitibu ama wanakula dawa ili wapone.
Licha ya
baadhi ya misemo na methari kama zile tulizofundishwa na walimu wetu katika shule za msingi na sekondari kwamba usipoziba ufa utajenga ukuta kuchukua nafasi katika jamii yetu bila sisi wenyewe kujitambua kuwa ni aina gani ya kuta tunapaswa kuziba nyufa zake, tunabaki kuwa mashuhuda wa milipuko ya magonjwa tusiyoyajua  mengine yakiwa yale ambayo tumeyazoea kama kipindupindu, kuhara na kuharisha.
Kutokana na jamii kujenga mazoea ya magonjwa  haya , jamii haiogopi mzagao wa takataka za namna mballi mbali kuenea hadi kuelekea kushinda juhudi za serikali za manispaa zinazo husika ikiwemo wasimamizi wake. Hili limekuwa tatizo sugu kutokana na wachafuzi wa mazingira kushindwa kutambua wajibu wao katika kutunza na kulinda mazingira. Baada ya kutoa huduma zao na wanapo wajibishwa huilaumu serikali kana kwamba serikali hiyo ndiyo inayo sababisha adha za namna hiyo.

Kwa mkoa ambao ni kitovu cha nchi kama Dar es salaam sidhani kama msimu wa matunda flani ndio ungekuwa chanzo cha kuchafuka mazingira katika maeneo husika ukiacha na yale yenye wakazi wengi  na maeneo yanayo kua kama Kariakoo, Mbagala,  soko la kuu la Ilala Rosana buguruni,Ubungo na  kwingineko.
Mzagao wa maganda ya nanasi na mahindi kwa sasa ni kero katika maeneo mbali mbali hasa masokoni  ambako bidhaa hiyo huanzia kabla ya kufikia watumiaji wa mwisho ambao kwao  hutegemea  hali za bidhaa hizo na uhitaji wa kuzitumia katika muda husika.
Inasikitisha sana kuona kuwa hata juhudu zilizo anzishwa na manispaa za jiji kuonekana kugonga mwamba  kwa suala la usafi wa mazingira ambayo  ni jukumu la kila mwana jamii tena halihitaji elimu ya namna yoyote katika kudhibiti mzagao wa takataka hizi ambazo ni tishio kwa afya hasa za watoto wetu na wake zetu ambao ndio wahanga wa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na kuhara.


Mwaka uliopita katika rikizo ya mwezi wa 12 nilifanikiwa kutembelea nchi za jirani hasa katika mipaka ya magharibi(Rwanda na Uganda). Nilifikia hatua ya kutamani kubaki nchini Rwanda  baada ya kukuta hali ya usafi nchini humo iko juu kiasi kwamba nilishindwa kutupa ganda la pipi ya ivory nikajikuta nimerudi nalo katika mfuko wa suruali yangu.  Katika mazingira ya viunga vya miji ya Rusumo na Karemela nje ya mkoa wa Kigali ambao ni kitovu cha nchi ya Rwanda (kama sisi, Dar es salaam.) usafi ndio salam inayo mkaribisha mgeni yeyote anae ingia kwa mara ya kwanza ama zaidi nchini Rwanda.
Nilitamani kuomba masomo ya ki ziara baada ya kurudi chuoni kwetu ili wenzangu wajifunze kwa kuona jinsi nchi ya Rwanda licha ya kuwa na historia ya machafuko ya  vita vya wenyewe kwa wenyewe,  ilivyo safi kiasi kwamba utadhani  mkoa wetu wa Dar es salaam. Unaonekana kama kijiji flani.
Jambo nililo jifunza ambalo linawezakuwa msaada kwetu ni kupunguza matumizi ya mifuko tunayoitumia katika mahemaezi yetu ya kila siku (mifuko laini maarufu ka ma Rambo.) mifuko hii haitumiki kabisa nchini Rwanda acha na kwetu ambako hata maji huuzwa katika mifuko hiyo.
Jambo lingine ni matumizi ya utii wa sheria za usafi, Rwanda haina kiongozi alie ju ya sheria,  wote huheshimu sheria. Kwamba kila Mnyarwanda anatambua umhimu wa usafi na jukumu lakekatika kuweka sehemu yake safi katika kujilinda mwenyewe na magonjwa yanayo sababishwa na uchafu.
Tuchukulie wauza maziwa ya ng’ombe hapa kwetu Tanzania kila muuzaji anatumia mbinu kuongeza kiasi cha maziwa kama kuongeza maji ama vingine lakini nenda Rwanda maziwa ya ng’ombe yanayo uzwa kama ni freshi haijarishi ni wapi yanako uzwa maziwa yoyote yanayo uzwa nchini humo hupimwa kwa kipimo maalumu (hygrometer) ili kuhakiki ubora wa maziwa kama yameongezwa kimiminika chochote muuzaji huwajibishwa pale pale hata kufikishwa mahakamani.
Hivyo licha ya ya mifuko hiyo laini kuwa kero katika mitaro inayotiririsha maji taka  bado kazi ya kudhibiti ubora wa bidhaa zetu nalo pia ni changamoto katika kuboresha usafi wetu na afya zetu. Katika hilo jamii inapaswa kujifunza kupitia makosa kwa kuwekwa sheria kali na wale wanaosimamia usafi  katika maeneo ya jiji letu kuisimamia kwa  kuilinda sheria hiyo, tatizo linalotukuta katika kutimiza huduma zetu ni mianya ya rushwa ambapo wenzetu wanapo kamatwa huwauliza walio wakamata kuwa ‘ukinifikisha huko unadhani utapata nini? Hivyo  mkamataji hulazimika kushawishika kupokea chochote  kutokana na ukweli kuwa  hakuna atakachofaidi tofauti na kuanzisha uhasama.
Achila mbali na sheria kali zilizopo kwa sasa katika kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa wanao jisaidia katika maeneo ya wazi na kusiko kuwa na vyoo bado adhabu kama hiyo inahitajika kwa wauza nanasi, maji ya mifuko maarufu kama kandoro, wauza maembe katika viunga vya barabara na masokoni pamoja na wauza vyakula katika maeneo yenye vumbi na harufu kali kama stendi za dala dala.
Hili pia likiambatana na udhibiti wa wauza vyakula, mama na baba lishe, katika maeneo yote ya nchi kwa kuwapima afya zao kabla na wakati wa kutoa huduma zao ikwa ni pamoja na kuzuia vibali kwa akina mama wanao nyonyesha kutoa huduma hizo, pamoja na wale ambao wanatoa huduma zao katika



mazingira ya uambukizo kama sehemu zenye  magari hasa maeneo ya stendi ambako vumbi huchafua mazingira kwa kiasi kikubwa na kusababisha kuenea kwa  magonjwa kama kukohoa na mafua.
Si magonjwa hayo tuambayo tuna paswa kuyaepuka katika kulinda usafi wa nchi yetu na kuzuia kabisa kwa faini na kifungo tena ikibidi zawadi nono kutolewa kwa mwana mgambo anae fanikisha kumfikisha muuza maji ya mifuko anae bainika akiuza maji hayoau muuza vyakula ambae hufanya biashara katika maeneo ya hatari kwa afya za watumiaji.
Ni majipamoja na matunda  hayohayo yanayo uzwa katika mazinggira machafu  ambayo husababisha milipuko ya magonjwa ambayo hugalimu matibabu  lakini kutokana na kuogopa kuonekana wabaya wasimamizi wa usafi wa jiji hasa Dar es salaam hushindwa kuwa zuia kwa maneno kwamba hawana jinsi. Lakini je tulisha wahi kuhakikisha usalama wa maji hayo?  Maji hayo wakati mwingine huchotwa katika mitaro ambako kila aina ya uchafu hutupwa kisha kupakiwa katika mifuko ambayo nayo pia ni safi lakini si salama kwa asili. Hivyo ili kudhibit usafi na sisi tukafanana na jirani zetu ni jukumu la kila mtu kutambua mchango wake katika kutunza mazingira yak e na jamii inayomzunguka bila kushurutishwa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA