Tuesday 7 July 2015

ZIMBABWE YAIUZIA CHINA TEMBO 24

Wanaharakati wa kutetea maslahi ya wanyama wameishutumu hatua hiyo
Zimbabwe inasema inahitaji fedha kukabiliana na uwindaji haramu, lakini mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama yameghadhabishwa na hatua hiyo.
Waziri wa mazingira Zimbabwe amesema tembo hao walisafirishwa kwa ndege hadi China kwenye ndege binafsi ya mizigo.
Wahifadhi wanyama wanasema tembo wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake na kwahivyo kuwatenganisha tembo hao wadogo kutoka jamii zao katika umri mdogo ni kitendo cha ukatili na kitakacho kuwa na athari kubwa kwa wanyama hao.
Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini - Guangzhou. Inasemekana kwamba wanyama katika mbuga hiyo wanateswa na kuwekwa katika mzingira mabaya.
Raia wengi wa Zimbabwe wanaona tembo kama wanyama waharibifu wanaoharibu mazao na kuangusha miti.
-BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA