 |
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Roberto Jarrin akielezea namna TBL inavyopiga hatua katika uendeshaji na utoaji wa huduma zake nchini Tanzania |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya TBL
Ndugu Roberto Jarrin ameendesha warsha wa kibiashara katika chuo kikuu cha
kumbukumbu ya Stefano Moshi kampasi ya mjini mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa mzungumzaji mkuu katika
warsha hiyo iliyohudhuriwa na waadhiri,wafanya kazi pamoja na wanafunzi wa chuo
hicho,mkurugenzi mtendaji huyo aliye ambatana na meneja wa mambo ya nje na mawasiliano
TBL Bi Emma Oriyo na afisa masoko TBL kanda ya kaskazini mashariki Ndugu Devis
Deogratius, alianza kwa kutambulisha bidhaa mbalimbali ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo na
kuonesha namna TBL inavyopiga hatua katika kujikuza kama kampuni.
 |
Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi wakisikiliza kwa makini Mkurugenzi wa TBL Roberto Jarrin |
Akielezea kuhusu masoko Ndugu
Jarrin alielezea namna kampuni hiyo inavyojiendesha katika nchi za Afrika
pamoja na aina za bidhaa kulingana na maeneo husika ikiwa ni pamoja na
changamoto wanazokutana nazo na namna kampuni inavyokabiliana nazo na hasa
ikiwa ni upatikanaji wa malighafi kutoka kwa wakulima akitoa mfano kuwa Uganda
ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa malighafi katika ukanda wa Afrika
Mashariki.
 |
Taswira ya ukumbi na wahudhuriaji ilivyokuwa wakati wa warsha hiyo |
Akijibu maswali ya wanafunzi
waliotaka kujua namna TBL inavyotoa nafasi za ajira kwa wasomi na jinsi kampuni
inavyolichukulia suala la rushwa katika utoaji wa ajira Ndugu Jarrin alisema
“TBL inathamini wasomi wa nchi hii na inawapa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa
kazi katika kwa njia za tarajali lakini pia mpaka sasa imeweza kutoa ajira kwa zaidi ya watanzania 100,000, Vile vile kuhusu
rushwa hili ni tatizo lenye sura ya kipekee tunajitahidi kama kampuni kuajiri
mtu kwa kuwa anambinu za kazi na sii vinginevyo”.
 |
Afisa masoko TBL kanda ya kaskazini mashariki Devis Deogratius akizungumzia mchakato wa ajira kwa wasomi nchini Tanzania |
Akikazia kuhusu maelezo hayo
afisa masoko TBL kanda ya kaskazini mashariki Ndugu Devis Deogratius alisema
kuwa wasomi wengi wanajisahau kuwa elimu wanazopata hazitoshi wao kuonekana
bora katika ushindani wa soko la ajira hivyo wanahitaji kuweka jitihada zaidi katika kujishighulisha na kudhihirisha ubora
wao katika utendaji huku akitoa mfano wake kwa namna alivyoajiriwa na TBL mwaka
2007 na kwa jitihada na nidhamu ya kazi aliyoonesha aliweza kuendelezwa kielimu
nchini Afrika ya kusini na sasa kuwa afisa masoko TBL kanda ya kaskazini mashariki.
 |
Mhadhiri wa chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi Dr.Gasper mpehongwa akitoa neno la shukrani wakati wa warsha hiyo |
Akizungumzia warsha hiyo mhadhiri
wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Stefano Moshi Dr.Gasper Mpehongwa alishukuru na
kusifu ushirikiano uliopo kati ya TBL na chuo hicho kwa kuleta elimu hii chuoni hapa “Elimu
iliyotolewa kupitia warsha hii imekuja katika kipindi kizuri hasa ambapo
wanafunzi walikuwa wakijiuliza namna ya kupambana na soko la ajira ,ni
matumaini yangu mbegu hii iliyopandwa katika fikra za wanafunzi hawa itazaa
matunda mema”.
 |
Victor Kajuna mwanafunzi mwaka wa tatu akimuuliza swali Mkurugenzi mtendaji wa TBL Roberto Jarrin katika warsha hiyo |
Victor Kajuna mwanafunzi mwaka wa
tatu alipongeza kampuni ya TBL kwa hatua iliyopiga na kufanikiwa kugusa maisha
ya watanzania wengi kupitia huduma zake na kwa kuwa na mchango mkubwa kwa pato
lataifa kupitia kodi huku.Sambaba na hilo Sebastian Femba mwanafunzi mwaka wa
aliesema kuwa warsha hii licha ya kumpa nafasi ya kuifahamu TBL kwa upana
imempa changamoto ya kujituma hususani akijipanga kukabiliana na ajira pindi
atakapohitimu masomo yake.
 |
Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano TBL Bi Emma Oriyo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa warsha hiyo |
Alipokuwa akizungumzia suala la
kujipanga na changamoto za ajira kwa wasomi meneja wa mambo ya nje na
mawasiliano TBL Bi Emma Oriyo alisema “ili kuwa na mafanikio katika soko la
ajira ni kujijiengea uwezo wa haraka kumudu mabadiliko ya fikra kwani hilo
litakutofautisha wewe na wengine”.
 |
Mkurugenzi mtendaji wa TBL Roberto Jarrin akizungumza na mmoja wa wahudhuriaji wa warsha hiyo mara baada ya kumalizika |
 |
Meneja wa mambo ya nje na mawasiliano TBL Bi Emma Oriyo akiwa na Mhadhiri wa chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi Dr.Gasper mpehongwa wakielezea uhusiano uliopo baina ya TBL na chuo hicho |
 |
Mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha kumbu kumbu ya Stefano Moshi Frank Chang'a akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi |
Warsha hiyo ni ya kwanza
kufanyika chuoni hapo kwa kushirikisha
waadhiri,wafanya kazi pamoja na wanafunzi wa chuo hicho na imekuja kufuatia
ushirikiano uliopo kati ya TBL na chuo cha Stefano Moshi uliodumu kwa takribani
miaka nane sasa.
Na Dickson Mulashani wa FUNGUKA LIVE BLOG
0 comments:
Post a Comment