Saturday 1 August 2015

AZAM FC USO KWA USO NA GOR MAHIA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Image result for azam fc

Fainali ya Kombe la Kagame 2015 itazikutanisha timu za Azam FC toka nchini Tanzania dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.




Azam FC imekuwa ya pili kuingia fainali kwa kuitwanga KCCA kwa bao 1-0 huku Gor Mahia ikiwa imetangulia baada ya ushindi dhidi ya timu ngumu ya Al Khartoum.

Hii ni mara ya pili kwa Azam FC kuingia fainali ya Kagame, mara ya kwanza ikiwa ni 2012 ambapo ilifungwa na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Tom Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.

Mechi ya fainali itachezwa Jumapili, ikitanguliwa na ile ya mshindi wa tatu kati ya KCCA dhidi ya Al Khartoum.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA