ROONEY APIGA HAT TRICK MAN UNITED IKIITWANGA CLUB BRUGES 4 MTUNGI
Kama ulikuwa unaamini Wayne Rooney amefulia, basi ulijichanganya. Amepiga bao tatu au hat trick na kuihakikishia Manchester United kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Rooney ambaye alikuwa akiandamwa na ukame wa mabao, amepiga zote tatu, huku Herrera akipiga moja katika ushindi wa Manchester United wa mabao 4-0 dhidi ya Club Bruges ya Ubelgiji iliyokuwa nyumbani.
Mchezo wa kwanza Man United ilishinda kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani Old Trafford, lakini leo imeshinda nne na kusonga mbele na ushindi wa mabao 7-1.
Angalia picha za action.
0 comments:
Post a Comment