Thursday 27 August 2015

SALVA KIIR ATIA SAINI MKATABA WA AMANI:SUDAN

Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametia saini makubaliano ya amani yanayonuiwa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda wa miezi ishirini.
Bwana Kiir, ambaye alikataa kutia saini mkataba huo wiki iliyopita amesema bado hana imani kamili kuhusu mkataba huo.
Usitishwaji wa mapigano unapaswa kutekelezwa katika muda wa saa 24 na majeshi ya kigeni yanapaswa kuondoka nchini humo.
Sudan Kusini
Hakuna wanajeshi watakaoruhusiwa kufika karibu na mji mkuu Juba.
Kiir ambaye alikabiliwa na shinikizo za kimataifa kuidhinisha mkataba huo anatarajiwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kiongozi wa waasi Riek Machar.BBC

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA