Friday, 28 August 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka mtandao wa matapeli wanaojipatia fedha kutoka kwa wananchi kwa udanganyifu kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi hasa katika kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi lipo katika mchakato wa ajira.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na mtandao wa matapeli hao na kwamba, mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na unafuata taratibu na kanuni za Jeshi la Polisi, hivyo, Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi hilo wafuate maelekezo yaliyoainishwa katika matangazo ya ajira yaliyotolewa kupitia vyombo vya habari pamoja na tovuti ya Polisi ya www.policeforce.go.tz ili kuepuka usumbufu na utapeli wa wahalifu hao.
Tunawakumbusha vijana wote waliochaguliwa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa kabla hawajaripoti shule ya Polisi Moshi. Hivyo, yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa kamanda wa mkoa anakotoka hatapokelewa chuoni.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA