Thursday 10 September 2015

UZINDUZI WA KAMPENI ZA URAIS WA ZANZIBAR (CUF), VIWANJA VYA KIBANDA MAITI ZANZIBAR.



Na: Hassan Hamad (OMKR)
 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema bado ndoto yake ya kuimarisha uchumi wa 
Zanzibar na kuifanya kuwa Singapore ya Afrika Mashariki iko pale pale.
 
Amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watamchagua na kumpa ridhaa ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu ujao, atauimarisha uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa kuufanya kuwa na sehemu ya mizigo ya kimataifa, ili kuwazesha wafanya biashara wa Afrika Mashariki kupokea mizigo yao Zanzibar badala ya kuifuata Dubai.
 
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza hayo leo wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa CUF na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA, katika mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni za Urais wa Zanzibar kupitia CUF.
 
Sambamba na hilo amesema iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar, atahakikisha kuwa suala la mafuta na gesi asilia halitoendelea kuwa hadithi, na badala yake ataunda Wizara ya Mafuta na Gesi, ili suala hilo liweze kufanyiwa kazi ndani ya siku mia moja za mwanzo za uongozi wake.
 
Amefahamisha kuwa serikali yake pia itaanzisha benki ya uwekezaji ya Zanzibar, ili kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
 
Maalim Seif ameongeza kuwa ndani ya miaka mitano ya mwanzo ya uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, ataweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza Zanzibar, na kuwawezesha vijana kuondokana na tatizo la ajira linalowakabili kwa muda mrefu sasa.
 
Akizungungumzia kuhusu Katiba, Maalim Seif amesema kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa Ukawa upande wa Tanganyika iwapo watachaguliwa kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watahakikisha kuwa wanairejesha katiba iliyopendekezwa na wananchi yenye muundo wa 
Muungano wa serikali tatu, na kuzipatia Zanzibar na Tanganyika mamlaka yake kamili.Kuhusu viongozi wa UAMSHO wanaoshikiliwa Tanzania Bara, 
 
Maalim Seif amesema Zanzibar ikipata mamlaka yake kamili chini ya uongozi wa CUF, watawarejesha viongozi hao ili kesi yao isikilizwe Zanzibar badala ya kusikilizwa Tanzania Bara.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA