BAO LA SAMATTA LAIBEBA MAZEMBE KUWANIA UBINGWA AFRIKA
Mtanzania Mbwana Samatta ameiweka klabu yake ya TP Mazembe katika nafasi nyingine ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufunga bao muhimu.
Licha ya kuwa ugenini, TP Mazembe ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Rainford Kalaba katika dakika ya 27 lakini dakika ya 45 Mzambia huyo akatolewa kwa kadi nyekundu.
Kipindi cha pili, TP Mazembe walionyesha kuwa makini wakilinda lbao lakini walimtumia Samatta kuendelea kuwasumbua walinzi wa USM Alger.
Dakika ya 68, Hocine El Orfi alilambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu.
Dakika ya 79, Samatta akafanya yake baada ya kufunga bao la pili na kuiweka Mazembe katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano Novemba 8 mjini Lubumbashi.
Hata hivyo wenyeji walionekana kutokata tamaa hadi walipopata bao moja katika dakika ya 88 kupitia kwa Mohammed Seguer.
0 comments:
Post a Comment