MOTISHA!! WAFANYAKAZI WA TBL GROUP WATUNUKIWA VYETI VYA UFANISI
Mkurugenzi
wa kampuni ya TBL Group,Roberto Jarrin akiwa katika picha na baadhi ya
wafanyakazi waliotunukiwa tuzo ya you Make the Difference katika
kiwanda cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group, Roberto Jarrin (Kushoto) akiwa na mfanyakazi wa
kitengo cha ufundi wa kiwanda cha Mbeya Godwin Kambi baada ya kumtunukia
cheti kwa kufanyia kazi kiwandani hao kwa kipindi cha miaka 15.Hafla
ya kuwatunuku wafanyakazi vyeti ilifanyika hivi karibuni kiwandani hapo.
Margaret
Simon Mlwale ambaye ni Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Darbrew naye amepata cheti cha kutambua mchango wake kwa
kampuni,waliosimama nyuma yake kutoka kulia ni Afisa Mwandamizi wa
utawala Phinias Mashauri,Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin na
Mkurugenzi Mkuu wa DarBrew David Cason,DarBrew iko chini ya TBL Group.
Mfanyakazi wa Arusha Anna Andrew ni miongoni mwa waliotunukiwa cheti cha kutambua mchango wake kwa kampuni.
Mfanyakazi
wa kiwanda cha Konyagi Ephreim Mwaswala akiwa ameshikilia cheti cha
utambuzi wa mchano wake kwa kampuni alichotunukiwa na Mkurugenzi Mkuu wa
TBL Group, Roberto Jarrin (Kulia) katika hafla iliyofanyika kiwandani
hapo hivi karibuni.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kiwanda cha Konyagi
Joseph Chibehe.
Wafanyakazi
wa TBL Group wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin muda mfupi baaa ya kuwatunukia vyeti
vya kutambua mchango wao wa kazi kwa kampuni .Hafla ya kukabidhi vyeti
imefanyika hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Deocracius Damas naye alipewa cheti cha kutambua mchango wake wa kazi kwa kampuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya TBL
Group, Roberto Jarrin, ametoa vyeti vya ufanisi (you Make the
Difference) kwa wafanyakazi bora katika kipindi cha robo ya mwaka huu
ikiwa ni utaratibu wa kampuni kutoa motisha kwa wafanyakazi wake
wanaofanya vizuri.
Wafanyakazi hao walichaguliwa katika viwanda vya kampuni hiyo vilivyopo Dar e salaam,Mwanza,Arusha na Mbeya,na hafla za kuwatunukia vyeti zilifanyika hivi karibuni katika viwanda hivyo.
Wafanyakazi hao walichaguliwa katika viwanda vya kampuni hiyo vilivyopo Dar e salaam,Mwanza,Arusha na Mbeya,na hafla za kuwatunukia vyeti zilifanyika hivi karibuni katika viwanda hivyo.
0 comments:
Post a Comment