LIGI KUU KUENDELEA JUMAMOSI HII
Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo
saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa
kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.
Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam Jumamosi hii, Simba SC watawakaribisha
African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC uwanja wa Karume,
huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu,
Turiani mkoani Morogoro.
Jijini
Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans
uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja
wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya
Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo
itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo Maafande wa Mgambo
Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga.
0 comments:
Post a Comment