SIMBA MWENYE MENO KICHWANI AONEKANA MAREKANI
Simba huyo alikuwa pia na masharubu ya ziada
Simba wa milimani aliyeuawa katika jimbo la Idaho, nchini
Marekani ameshangaza wengi kutokana na hali kwamba alikuwa na meno ya ziada
kichwani.
Meno hayo kamili yanachomoza kutoka kwenye paji la uso na
kuonekana kama pembe.
Simba huyo aliuawa na wawindaji walioidhinishwa tarehe 30
Desemba.
Idara ya Wanyamapori na Samaki ya Idaho imesema meno hayo
huenda ni masalio ya pacha ambaye labda alifariki akiwa tumboni, au labda
inatokana na saratani.
Wataalamu wa vimbe katika jimbo hilo wanasema hawajawahi
kuona ulemavu wa aina hiyo awali.
Simba huyo aliwindwa na kuuawa baada ya kumshambulia mbwa
karibu na mji wa Weston. Mbwa huyo alinusurika lakini mwindaji akatumwa
kumuwinda simba huyo na kumuua.
Afisa wa uhifadhi wa wanyama alikagua mzoga wa simba huyo
kama ilivyo sheria na ndipo akagundua meno hayo.
Mnyama huyo pia alikuwa na masharubu kwenye paji la uso kushoto
0 comments:
Post a Comment